June 17, 2017

RAIS WA TAIFA LA VANUATI AFARIKI DUNIA

Rais wa Visiwa vya Vanuatu afariki dunia

Rais wa visiwa vya Vanuatu, Baldwin Lonsdale wakati wa uhai wake 

Vanuatu. Rais wa visiwa vya Vanuatu, Baldwin Lonsdale amefariki dunia kwa kile kinachodaiwa kuwa ni mshtuko wa moyo leo.
Lonsdale ambaye pia ni Kasisi wa Anglikana amekuwa kiongozi wa kisiwa hicho cha Pacific kwa miaka miwili tangu Septemba 2014.
Gazeti la Daily Post nchini Vanuatu limesema kuwa Lonsdale alifariki ghafla kwenye mji mkuu wa Port Vila usiku wa kuamkia leo.
Akiwa rais, Lonsdale aliongoza ujenzi mpya wa maeneo ya kisiwa hicho kufuatia uharibifu uliosababishwa na kimbunga cha Pam kilichosababisha watu 75,000 kukosa makazi mwezi Machi mwaka 2015.
Oktoba mwaka huohuo aliapa kupambana na ufisadi nchini humo baada ya sakata lililomhusisha makamu wake la matumizi mabaya ya rasilimali za umma.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE