June 6, 2017

RAIS MAGUFULI AWAMAPISHA VYEO MAOFISA WAKE


unnamed


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mh. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amewapandisha vyeo Maafisa watano wa Magereza kuwa Naibu Makamishna  na  wengine 24 kuwa Makamishna Wasaidizi Waandamizi  wa Magereza kuanzia tarehe  25 mwezi Mei, 2017.
Waliopandishwa vyeo kuwa Naibu Kamishna wa Magereza ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Uwesu H. Ngarama,  Boharia Mkuu wa Jeshi la Magereza, Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Gideon M. D. Nkana, Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Ukonga, Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Jeremiah .M.C. Nkondo,  Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kagera, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Tusekile S. Mwaisabila, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Lindi pamoja na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Augustine S. Mboje ambaye ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam.
Waliopandishwa vyeo kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza ni Kamishna Msaidizi wa Magereza Mbaraka Sultan Semwanza, Mwalimu wa Hisabati na Kemia shule ya Sekondari Bwawani inayosimamiwa na Jeshi Magereza, Kamishna Msaidizi wa Magereza George Togholai Mwambashi, Mkuu wa Kitengo cha Sheria Makao Makuu ya Magereza Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza Charles R. Novat, Mkuu wa Kitengo cha Mafunzo Makao Makuu ya Magereza Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza Faustine Martin Kasike Mkufunzi Mwandamizi Chuo cha Ulinzi wa Taifa (NDC) Kunduchi Dar es Salaam.
Wengine ni Kamishna Msaidizi wa Magereza Joel Silverster  Bukuku, Mdhibiti wa Shirika la Magereza, Kamishna Msaidizi wa Magereza Deogratius Ndaboine Lwanga, Afisa Mnadhimu, Magereza Makao Makuu Ukonga, Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza Boyd Patric Mwambingu, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi wa Magereza Athuman Ambayuu Kitiku, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Magereza Hassan Bakari Mkwiche,  Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Magereza Luhende DAVID Makwaia, Mkufunzi Mkuu wa Mafunzo ya Kijeshi na Msaidizi wa Mkuu wa Chuo cha Magereza Kiwira Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Magereza Hamza Rajab Hamza, Afisa Mnadhimu wa Magereza Mkoa wa Tabora na Kamishna Msaidizi wa Magereza Jeremiah Yoram Katungu, Msaidizi Ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Magereza Makao Makuu Dar es Salaam.
Wengine ni Kamishna Msaidizi wa Magereza Mzee Ramadhan Nyamka, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Magereza Afwilile Mwakijungu, Mkuu wa Gereza Isupilo Mkoa wa Iringa,  Kamishna Msaidizi wa Magereza Ally Abdallah S. Kaherewa, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Ruvuma, Kamishna Msaidizi wa Magereza Salum Omar Hassan, Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Magereza Ismail T. Mlawa, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mtwara, Kamishna Msaidizi wa Magereza Chacha Bina Jackson, Mdhibiti wa Fedha Makao Makuu ya Magereza Dar es Salaam na  Kamishna Msaidizi wa Magereza Rajab Nyange Bakari, Mkuu wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Ghasia Magereza Ukonga Dar es Salaam.
Wengine ni Kamishna Msaidizi wa Magereza Kijida Paul Mwankingi, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Magereza Julius Cosmas Ntambala, Msimamizi Mkuu wa Ujenzi wa Nyumba 320 za Kuishi Askari Gereza la Ukonga, Kamishna Msaidizi wa Magereza Mussa Musuluzya Kaswaka, Afisa Mkaguzi Makao Makuu Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza Justine M. Kaziulaya, Mratibu Msaidizi Baraza la Usalama la Taifa na  Kamishna Msaidizi wa Magereza Bertha Joseph Minde ambaye ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Manyara.    

Imetolewa na
Meja Jenerali Projest Rwegasira
Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 
6 Juni 2017

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE