June 22, 2017

RAIS MAGUFULI AMSIFU KIKWETE UTEKELEZAJI WA SERA YA VIWANDA


Dar es Salaam. Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete amesema jimbo hilo limeweka historia kwa kuwa na viwanda jambo ambalo limewezekana baada ya Rais John Magufuli kuingia madarakani.
Ridhiwani amesema tayari kuna maandalizi ya kujengwa viwanda saba ndani ya miaka miwili tangu Rais Magufuli alipoingia madarakani.
"Mheshimiwa Rais (Magufuli) utaweka historia katika halmashauri yetu, haikuwa na kiwanda chochote ila leo hii tunaona viwanda saba vimeanza kujengwa ndani ya kipindi ulichopo madarakani, ni historia pekee kwako,"amesema.
Kauli hiyo ameitoa leo (Alhamisi) wakati wa uzinduzi wa Kiwanda cha kusindika Juisi cha Sayona kilichojengwa katika Kijiji cha Mboga, Kata ya Msoga, jimboni humo.
"Mambo tuliyoyafanya katika utekelezaji wa Ilani ya chama (CCM) tangu tulipoingia madarakani, kwanza tumetoa ile asilimia 10 ya kuwawezesha akina mama na vijana katika halmashauri yetu na sasa zaidi ya Sh200 milioni zimeshatolewa, halmashauri tumekusanya asilimia 102 ya mapato na hilo linatafsiri kaulimbiu yako ya ‘Hapa Kazi tu’," amesema.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE