June 23, 2017

RAIS DKT MAGUFULI ATOA MSAADA WA CHAKULA KWA YATIMA IRINGA ,OFISI YA RC IRINGA YAMUUNGA MKONO

Mkuu  wa  mkoa wa  Iringa  Amina Masenza  kushoto  akikabidhi  msaada  wa chakula  uliotolewa na Rais Dkt Magufuli na ofisi ya  mkuu  huyo wa  mkoa kwa  ajili ya Idd kwa  watoto  yatima  Dhi Nureyn  Iringa 
watoto  Yatima  wa  kituo cha  Tosa Maganga   wakimsikiliza  mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza 
Mkuu  wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza katikati  akitoa  msaada wa  chakula kwa  yatima  Tosamaganga  anayepokea ni mlezi wa  kituo  hicho  Sir Winfrida Mhongole  na  kushoto ni  katibu tawala  mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu 
Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Amina Masenza  kulia  akikabidhi  mbuzi  iliyotolewa na rais 
Watoto  Yatima  wa  vituo  vya  Dr Bilaal na  Dar  Fatma  wa  kituo cha  Dhi Nureyn  wakijiandaa  kupokea msaada wa  chakula  cha  Idd 
Mkuu  wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza  akizungumza na  watoto wa Dhi Nureyn 
Mkuu  wa  mkoa akikabidhi  msaada wa  mbuzi kwa  ajili ya  Idd 
Msaada  wa  mafuta  ya  kupikia 
Msaada wa  sabuni  kwa  yatima 
Na MatukiodaimaBlog 
RAIS wa  jamhuri ya  muungano  wa Tanzania  Dkt  John  Magufuli ametoa  msaada  wa chakula na mbuzi  kwa  yatima mkoani Iringa kwa ajili ya  sikukuu ya  Idd.

Akikabidhi  msaada  huo leo  kwa niaba ya  rais Dkt Magufuli mkuu  wa  mkoa wa  Iringa Amina Masenza alisema kuwa msaada  uliotolewa ni mchele kilo 150,mbuzi  mmoja  na mafuta  ya  kula rita  20,sabuni katoni tano  pamoja na pipi  kwa  ajili ya  watoto  hao.

Mkuu   huyo  wa  mkoa  alisema kwa  kuwa msaada  huo  umetolewa  kituo cha Tosamaganga na  kuwa  ofisi yake  kwa  kumuunga mkono  Rais  imetoa msaada  kama  huo kwa  kituo  cha  Dar Bilaal  na Dar –Fatma vilivyopo  chini ya  Dhi-Nureyn  mjini  Iringa .

Aidha  mkuu  huyo wa  mkoa  alipongeza jitihada  kubwa  zinazofanywa na vituo  vya yatima  mkoani Iringa na  kuitaka  jamii ya  mkoa  huo kuachana na tabia ya kutupa watoto kwani  kwa  kufanya  hivyo  mbali ya  kumkosea Mungu  bado  alisema mkoa hautapenda  kuona  ongezeko la  watoto wanaoishi katika mazingira  magumu ambao  wametokana na kutupwa na  wazazi .

“ Tunatambua   kuwa  wapo  yatima  hapa ambao  wazazi wao  walitangulia mbele za  haki ila  wapo ambao  wameokotwa baada ya  kutupwa na  wazazi  wao ….sasa  nawaombeni  sana  wananchi  wote  tusaidiane  kuwafichua   wanaoitupa  watoto “

Masenza  aliwataka  pia  wananchi  wa  mkoa wa Iringa kuendelea  kuwachichua  watu  wanaobaka  ama  kulawiti  watoto ili  kuchukuliwa  hatua  kali za kisheria.

Huku  akiwataka  wazazi  kuendelea  kuwachunga  watoto  wao na  kuepuka kuwatuma dukani  majira ya  usiku  kwani  kwa  kufanya   hivyo  kutaepuka  watoto  hao  kuendelea  kubakwa na  watu hao  wasio  wema.

Wakishukuru  kwa  msaada  huo walezi  wa  kituo  cha Tosamaganga na   Dhi Nureyn  walisema  kuwa  wamefarijika  na  upendo ulioonyeshwa na Rais Dkt  Magufuli  kwa  kuwajali  yatima na  kuwa   kazi yao  kuendelea  kumuombea  zaidi .

Mlezi  wa  kituo  cha Dhi Nureyn  Ally  Ramadhan alisema  kuwa wanatambua  kazi  kubwa  inayofanywa na Rais katika  kuwatumikia  watanzania  ila bado  hajaacha  kuwasaidia yatima  hao  ili  nao  waweze  kusherekea  Idd kama  watoto  wenye  wazazi  wao .

Huku Mlezi wa  kituo  cha  Tosamaganga  Sir  Mhongole  alisema  kuwa  bado  wanaomba  wadau  wengine na  viongozi  wengine  kuendelea  kumuunga mkono Rais kwa  kuwakumbuka yatima  katika maeneo  yao. 


MWISHO 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE