June 2, 2017

NDESAMBURO KUZIKWA JUMANNE IJAYO

Mbunge wa zamani wa Moshi Mjini (Chadema), Philemon Ndesamburo enzi za uhai wake

Moshi. Mbunge wa zamani wa Moshi Mjini (Chadema), Philemon Ndesamburo aliyefariki dunia jana atazikwa Jumanne ijayo.
Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa ameliambia gazeti hili kuwa Ndesamburo atazikwa katika makaburi ya familia nyumbani kwake eneo la Mbokomu.
Golugwa amesema Jumatatu, Juni 5 kwenye viwanja vya mashujaa mjini Moshi wananchi watapata fursa ya kuaga mwili wa Ndesamburo.
Katibu huyo amesema wakati wa kuaga mwili wake kutakuwa na salamu kutoka kwa viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, viongozi wa dini na wawakilishi wa makundi mbalimbali.
Golugwa amesema msiba wa Ndesamburo umewagusa wengi nchini kutokana na mchango wake katika kukuza misingi ya demokrasia ya vyama vingi na kuchangia ustawi wa sekta ya utalii.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE