June 3, 2017

NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA ATUA IRINGA KIKAZI

Naibu  katibu  mkuu wa  CCM Bara Rodrick Mpogolo akiongea na  viongozi  wa CCM mkoa wa Iringa  leo
Rodrick Mpogolo akizungumza na  viongozi wa CCM mkoa wa  Iringa

Rodrick Mpogolo skizungumza na viongozi  wa  CCM mkoa


Viongozi wa CCM mkoa  wa  Iringa  wakiwa  katika  kikao  pamoja na  naibu katibu mkuu

Katibu wa  UVCCM mkoa  James  Mgego  kushoto  akiwa na  viongozi  mbali mbali  wakati wa  kikao  na naibu katibu  wa CCM Tanzania Bara
NAIBU  Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo kesho  kuwa  mgeni  rasmi katika maafali ya  wana CCM yatakayofanyika  katika ukumbi wa Siasa  ni kilimo mjini Iringa .


Katibu wa UVCCM  mkoa  wa  Iringa  James  Mgego  amesema   kuwa  tayari  naibu katibu  mkuu  wa  CCM amewasili mjini  Iringa na  kuwa  shughuli  hiyo ya  maafali  kwa  wana CCM 211itaanza mapema kesho asubuhi .


Mgego alisema   wakati  maafali  hayo  yanafanyika  vijana  wa UVCCM mkoa  wa  Iringa  wapo katika  harakati  za kuhamasisha  wana  CCM wakiwemo vijana  kujitokeza kuwania nafasi  mbalimbali za uongozi ndani ya ya  CCM wakati  huu ambao  chaguzi zinaendelea  ndani ya  chama .


Hata  hivyo  Mgego  alisema  ujio wa  naibu katibu mkuu wa CCM Tanzani bara  ndani ya mkoa  wa  Iringa  kwa vijana na  chama ni  hatua  nzuri  kwa  wasomi hao  kuangalia  namna ya kuendeleza  umoja  na  hamasa ya kuwafanya  wengi  kushiriki kugombe nafasi za uongozi .0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE