June 21, 2017

MWILI WA ALLY YANGA KUAGWA LEO DODOMA

MWILI wa  aliyekuwa shabiki maarufu wa klabu ya soka ya Yanga Ally Mohammed almaarufu Ally Yanga unatarajiwa kuagwa leo katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kabla ya kuelekea Shinyanga kwa mazishi.

Marehemu Ally Yanga
alifariki jana kwa ajali ya gari iliyotokea kijiji cha  Chipogolo wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.

Shughuli ya kuuaga mwili wa Marehemu Ally Yanga zinatarajiwa kufanyika eneo la Mochwari na  kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri,viongozi wa  chama na serikali.

Enzi za uhai wake marehemu Ally Yanga  mbali na kuwa shabiki na mhamasishaji wa timu ya Yanga alikuwa shabiki  wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) na shabiki wa shughuli za serikali kama Mwenge wa Uhuru na ziara za viongozi.

Mwenyezi Mungu aipokeee roho ya marehemu Ally Mohammed na kuiweka mahali pema peponi Amin.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE