June 6, 2017

MWIGAMBA KUMRITHI ZITTO KABWE ACT

Chama cha ACT-Wazalendo kimemteuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni na Uchaguzi Samson Mwigamba kuwa Kaimu Kiongozi wake na kufanya shughuli zote za Kiongozi wa Chama, Zitto Kabwe ambaye ameanza safari ya siku kumi kwenda nchi za Uingereza, Ujerumani, Sweden na Denmark kwa safari za kichama kwa kipindi chote ambacho Kiongozi huyo atakuwa nje ya nchi.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyitolewa leo Juni 6, 2017 na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma, ACT Wazalendo Ado Shaibu, inaeleza kuwa madhumuni ya safari hiyo ni kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Chama cha Die Linke cha Ujerumani.
Ambapo pia atafanya mazungumzo na viongozi wa vyama rafiki barani Ulaya ili kuimarisha mahusiano baina ya ACT na vyama hivyo.
“Kwa mujibu wa Ibara ya 29(25)(xi) ya Katiba ya ACT Wazalendo, tumemteua Mwigamba kuwa Kaimu Kiongozi hadi pale kiongozi Mkuu atakaporejea. Tunamtakia Ndugu Samson Maingu Mwigamba utekelezaji mwema wa majukumu yake,” inaeleza taarifa hiyo.
Na Regina Mkonde

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE