June 13, 2017

MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU WATOA TAARIFA YA KUFIKISHWA MAHAKAMANI MRATIBU WAKE .........Mratibu  wa  mtandao  wa watetezi wa haki za  binadamu  Onesmo  Ole  Ngurumo (wa  pili  kulia)  akiwa na watetezi  wenzake na wanasheria  leo

Leo tarehe 13 ya mwezi Juni 2017 Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania Ndugu Onesmo Olengurumwa amepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Mwanzo ya Magomeni na kusomewa mashtaka katika kesi ya jinai namba 645 ya mwaka 2017. Ndugu Onesmo ameshtakiwa kwa kosa moja la kuingia kwa jinai kinyume na kifungu cha 299 cha Kanuni ya Adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2010.

Mashtaka yamesomwa mbele ya Mh. Hakimu Patrick Vaginga ambapo mtuhumiwa amekana kosa hilo na hivyo kuachiwa huru kwa dhamana hadi tarehe 27mwezi Juni mwaka 2017 kesi itakapoitwa tena. Ili kuwa huru kwa dhamana Mh. Vaginga aliamuru mshtakiwa awe na wadhamini wawili na bondi ya shilingi milioni moja ambavyo mtuhumiwa alivitimiza na kuachiwa kuru.

Onesmo Olengurumwa alikamatwa na Polisi  juni tatu 2017 alipokua akijiandaa kuhudhuria uzinduzi wa kitabu kinachoitwa Sauti ya Watetezi wa Haki Vyuoni kilichoandikwa na Alphonce Lusako mwanafunzi aliyefukuzwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kutokana na jitihada zake za kutetea wanafunzi wa vyuo.
Imetolewa na THRDC
Leo tarehe 13 Juni 2017

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE