June 2, 2017

MNYIKA ALIVYOTOLEWA NJE YA BUNGE LEO

Panga la Spika wa Bunge kuadhibu wabunge ambao wamekwenda kinyume na taratibu na ukosefu wa nidhamu limemkuta Mbunge wa Kibamba , Mh. John Mnyika wa CHADEMA baada ya kuamuliwa kutoka nje ya bunge kwa kile kilichoelezwa kuwa ni utovu wa nidhamu.
Spika wa Bunge aliamuru walinzi wa Bunge kumtoa nje mbunge huyo na kusema hataruhusiwa kushiriki katika vikao vya bunge kwa siku 7, jambo ambalo limepelekea wabunge wengine wa upinzani kutoka nje ya ukumbi wa Bunge kupinga kitendo hicho alichofanya Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Akizungumza nje ya bunge Mbunge Ester Bulaya amesema kuwa kazi ya wabunge wa upinzani ni kuishauri serikali, hivyo wao hawawezi kuishauri serikali vile ambavyo inataka kushauriwa na kusema wapo wabunge wa Chama Cha Mapinduzi wamekuwa wakitumia lugha isiyo na staha lakini wamekuwa wakiachwa huku wabunge wa upinzani wakichukuliwa hatua kama hizo.
"Nadhani hata nyinyi mmeona mbunge aliyekuwa anachangia anasema kuwa wabunge wengine wapimwe akili, inawezekana hawana akili anaachwa kwa sababu tu ni mbunge wa Chama Cha Mapinduzi, msimamo wetu kama Kambi ya Upinzani tumeamua kutoka kwa sababu hatuwezi kujadili mambo ya msingi kwa kufanyiwa mambo haya, sisi kazi yetu ni kuishauri serikali lakini hatuwezi kuishauri serikali vile wanavyotaka wao. Kwenye Wizara ya Ardhi mbona wabunge wa upinzani walisimama na wakapongeza na Wizara ya Ardhi ilipita bila shida yoyote kwa pande zote mbili, sasa kwanini wao wanataka kupongezwa tu? Kazi yetu ni kuona pale ambapo mambo hayaendi sawa kwa mujibu wa sheria tunasema na hili liwe wazi watu waliokuwa wakipigia kelele mikataba mibovu ni upinzani bungeni" alisisitiza Ester Bulaya 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE