June 1, 2017

MFUKO WA PSPF WASAIDIA BATI ZA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA WILAYA YA KILOLO

Uongozi  wa  serikali ya  mkoa wa Iringa wakiongozwa na mkuu wa mkoa  wa Iringa Amina Masenza  (wa  tatu kushoto ) akifuatiwa na mkuu wa wilaya ya  Kilolo Asia Abdalah ,mkurugenzi wa Halmashauri ya  Kilolo Aloyce Kwezi,wakipokea msaada wa bati  120  zenye  thamani ya  zaidi ya  shilingi  milioni 2.4  kwa  ajili ya  kuunga mkono  ujenzi wa madarasa  wilaya ya Kilolo wa kwanza  kulia ni mkurugenzi wa Halmashauri ya  Mufindi Prof Riziki Shemdoe  na mkuu wa  wilaya ya Mufindi Jamhuri  Wiliam wakipokea  msaada  huo wa bati kutoka mfuko  wa PSPF kushoto  wa pili ni afisa mfawidhi  wa PSPF Baraka  Jumanne  wa  pili na Samwel Sawa
Wanahabari  wakimhoji  mkuu  wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza juu ya hali  halisi ya  ujenzi wa  vyumba  vya madarasa
Mkuu  wa  mkoa wa Iringa  Amina Masenza akiwapongeza  PSPF  kwa  msaada  wao 
MFUKO  wa Pensheni wa PSPF  mkoani  Iringa umetoa msaada  wa bati 120 zenye  thamani  ya shilingi milioni 2.4  kwa  uongozi wa mkoa  wa  Iringa kwa  ajili ya  kuunga  mkono  ujenzi wa vyumba vya madarasa 490  wilaya ya  Kilolo .

Akikabidhi  msaada  huo  leo  mbele ya mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza ,afisa mhifadhi wa PSPF mkoa wa Iringa Baraka Jumanne alisema  kuwa  mfuko   mfuko  huo  uliombwa na uongozi wa  wilaya ya  Kilolo kupitia mkuu wa wilaya   hiyo Asia Abdalah kusaidia bati kwa ajili ya ujenzi wa  vyumba vya madarasa.

Alisema  wao kama  miongon mwa  mifuko ya  Pensheni  nchini wanawajibu wa  kuendelea  kuunga  mkono  jitihada  za kimaendeleo zinazofanywa na serikali  ya awamu ya  tano  na  wataendelea kuunga mkono jitihada  hizo.

“  Tunaendelea  kusaidia  ili  kutekeleza  agizo la rais wetu  la  ujenzi wa vyumba vya madarasa ili  wanafunzi  wetu  waweze kusoma”

Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo  Asia Abdalah   pamoja na kupongeza msaada  huo  alisema  wilaya  yake inakabiliwa na  changamoto kubwa ya upungufu wa  vyumba  vya madarasa sekondari  madarasa 40 na shule  ya msingi  kuna upungufu wa  vyumba vya madarasa 450.

Hivyo  alisema  tayari wamewaangukia   wadau mbali mbali ili kusaidia  ujenzi wa  vyumba vya madarasa  kwa  kuchangia  vifaa vya ujenzi  na kuwa  tayari  wadau wameanza  kujitokeza  ikiwemo kampuni ya  Makota  forest  .

Mkurugenzi  mtendaji wa Halmashauri ya  wilaya ya  Kilolo Aloyce Kwezi alisema  kuwa  kumekuwepo  na  mwitikio  mzuri  kutoka kwa wadau mbali mbali  hasa  wawekezaji  waliopo  wilaya   hiyo kusaidia shughuli za kimaendeleo  na  kuwa bado wataendelea  kufanikisha  ujenzi wa  vyumba vya madarasa  kwa  kushirikiana na wadau hao .

Kwani  alisema miongoni mwa wadau wa maendeleo  waliopo Kilolo  ni pamoja na New Forest , Makota Forest ,Rutuba ,Mtanga  na  wengine  wengi na kuwa  kupitia  wao  wana mkakati wa  kuanza  kuboresha  pia mahabara  katika  shule  mbali mbali .
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina  Masenza alisema kuwa  hali ya  vyumba  vya madarasa  katika  mkoa wa Iringa  bado  si nzuri kwani  kuna upungufu mkubwa  na upungufu huo umesababishwa na ongezeko la  watoto  kujiunga na shule  za msingi kufuatia mpango mzuri wa  serikali ya awamu ya  tano  wa elimu  bila malipo .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE