June 14, 2017

MBUNGE KABATI AWACHANGISHIA PESA CHARUKUWA , ASEMA ATAZIDI KUWA SAIDIA YATIMA

Mbunge wa  viti maalum  mkoa wa Iringa  Ritta Kabati (CCM)  wa  tatu kushoto  akishiriki kukata  kike  wakati  wa  harambee ya  chama  cha kusaidia yatima na wasio jiweza chuo  kikuu  cha Augustino (RUCU) - CHARUKUWA 
Baadhi  ya wanachama  wa  CHARUKUWA
Wanachama  wa  CHARUKUWA wakimsikiliza  mgeni  rasmi
Wanachama wa  chama  cha  Charukua  wakifuatilia  hotuba ya  mgeni  rasmi
Meza kuu  ikiongozwa na  mbunge  Ritta Kabati kulia  wakifuatilia  burudani  toka kwa  wanachuo  RUCU
Utambulisho  kwa  viongozi  mbali  mbali  wa  chama  hicho 
Wanachama wakijiandaa  kwa  changizo
Mbunge  Kabarti  akipongezwa na  wanachuo  RUCU

Mbunge  Ritta  Kabati  akijiandaa kwa  shampeni
Mbunge Kabati  akipewa  Shampeni
Meneja  wa  uwanja  wa Ndege  Nduli  akitoa  ahadi ya mchango  wake
Kike  ya  changizo  ikiandaliwa
Mbunge  Kabati  akiwalisha  keki  wanachama wa  CHAUKUWA
Wanafunzi  wanaobaki  wa CHAUKUWA wakijiandaa  kuchangia
Na MatukiodaimaBlog
KATIKA kuunga mkono  jitihada za wanafunzi wa  chuo kikuu   kikuu  cha  Ruaha Iringa  (RUCU) kusaidia  yatima na  wenye  ulemavu  mbunge  wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa (CCM) Ritta Kabati  amechangisha   kiasi cha  zaidi ya shilingi  milioni 5 kusaidia  ujenzi wa jengo la kituo cha kutoa kutoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu na wenye uhitaji Isimila  wilaya ya Iringa .

Wanafunzi  wa chuo  hicho  kupitia  Chama cha Rucu cha Kuwasaidia Wahitaji (CHARUKUWA) ndio  ambao  waliandaa  harambee   hiyo  juzi na  mgeni  rasmi  kuwa  mbunge  Kabati ambae  alifanikisha  kupatikana  kiasi  cha  shilingi milioni 5.3 zikiwa  pesa taslim na ahadi .

Akizungumza mara  baada ya  harambee hiyo, mbunge  Kabati pamoja na kuwapongeza wanafunzi hao kwa kuanzisha chama  hicho  cha  kuwasaidia wenye uhitaji bado  alisema ofisi yake  ikiendelea  kuunga mkono jitihada  hizo za kuwasaidia watoto wanaoishi  katika mazingira magumu kwa kuwajengea nyumba ambayo  itakuwa msaada  mkubwa  kwao.
Mbunge  Kabati  alisema  kuwa kazi  inayofanywa na  wanafunzi hao ndio kazi  ambayo  alikuwa  akiifanya  yeye  kabla ya  kuwa  mbunge na baada ya kuwa  mbunge  kwani siku  zote  amekuwa akiamini  kuwasaidia  yatima na  wajane  na  wasio  jiweza  ni Baraka  kubwa  mbele za  Mungu na yeyote anayesaidia wao  hao hakosi  Baraka  .

Alisema pamoja na  kuwa ataendelea kuchangia  chama  hicho  ila kwa  sasa amelazimika kuchagia  shilingi milioni moja kwa  ajili ya kuanzisha  ujenzi  huo na mara  watakapoandaa gharama  kamili  atawaongezea  zaidi .

Mwenyekiti Mstaafu wa CHARUKUWA, John Banda alisema harambee hiyo itawezesha kupatikana kwa fedha za kuanza
ujenzi wa msingi wa kituo hicho ambapo jumla ya shilingi 3,000,000 zinahitajika
kabla ya kupandisha ukuta.
Alisema kuwa lengo la kuanzishwa kwa chama hicho ni kutoa
msaada kwa wahitaji ili walau kuwapa ahueni ya maisha, kutoa misaada kwa
makundi mbalimbali wakiwemo watoto yatima katika vituo vyao, wagonjwa walioko
hospitalini, katika vituo vya afya na walioko majumbani.

Aidha Banda alitoa wiyo kwa wadau mbalimbali kujitokeza
katika kuwachangia katika ujenzi wa kituo hicho cha watoto yatima ambapo fedha
wanazozichanga wao kama wanafunzi haziwezi tosheleza ujenzi wa kituo hicho
hivyo kuomba msaada kwa wahisani mbalimbali kuwasaidia katika malengo ya ujenzi
wa kituo hicho.
 
Kuanzishwa kwa  chama  hicho ni ukombozi  mkubwa kwa  watoto  yatima  mkoa  wa  Iringa ambao  ni  moja kati  ya  mikoa ambayo  inaidadi kubwa ya  watoto  yatima na  wale  wanaoishi  katika mazingira magumu  ambao  wametokana na  familia  zao  kutengana  ama  kupoteza maisha .

 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE