June 29, 2017

MBOWE-POLISI MSITUFUNGE MIDOMO YETU


Mwanyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amelitaka jeshi la polisi nchini kutowafunga midomo na kusema kitendo cha jeshi hilo kuwafukuza waandishi wa habari wakati wakifanya kazi yao si sawa. 
Freema Mbowe
Freeman Mbowe amesema hayo leo baada ya jeshi la polisi kuwafukuza waandishi wa h abari ambao walikuwa wakifuatilia tukio la kuwasili kwa Mhe. Edward Lowassa Makao Makuu ya Polisi ambapo leo alikwenda kuitika wito wa jeshi hilo baada ya jana kutoa maelezo na kutakiwa kufika leo tena.

Mhe Edward Lowassa alipata wito kutoka kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) kumtaka kufika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi siku ya Jumatano tarehe 28 kufuatia kauli zake alizozitoa ambazo zinasemakana kuwa ni uchohezi, Lowassa jana alifika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na kutoa maelezo yake kwa muda wa masaa manne, kisha baada ya hapo alijidhamini mwenyewe na kutakiwa kufika siku ya Alhamisi ya tarehe 29 Julai 2017 ambapo amefika na kuambiwa uchunguzi wa jambo lake haujakamilika hivyo arudi tena tarehe 13 Julai 2017.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE