June 8, 2017

MASHINDANO YA RITTA KABATI CHALLENGE CUP 2017 YAZIDI KUNOGA IRINGA , SASA ZAMU YA POLISI NA MSHINDO KUKABANA

Image result for Ritta Kabati  CupMASHINDANO ya  kombe la  Ritta  Kabati  Challenge Cup  2017  jumamosi    hii  yanaingia  hatua ya  mznguko  wa kwanza   huku  timu  za Mshindo  Fc  na  Polisi  Iringa  wakionyesha  kutambiana  kwa  kila  mmoja  kumfunga  mwenzake .
Uongozi  wa  timu ya  Mshindo  umesema kuwa unauhakika  wa   kuwalaza mahabusu  kwa  kuwagagadua  kama  si  kuwafunga  kwa  jumla ya  magoli  yasiyopungua  matatu  timu ya  polisi  Iringa ambayo  tayari  ilikwisha  fungwa   goli 3 -0  katika  mchezo  wao wa  kirafiki .
Kuwa   timu   hiyo  ya  Mshindo  ambayo  inajivunia kwa   kutokusajili  zaidi ya  wachezaji  kujipeleka  kutaka  kuichezea   timu   hiyo ,kuwa  wapo  vizuri  kutoa  upinzani  mkubwa  kwa  timu ya  polisi na ikiwezekana  ubingwa wa mashindano hayo ubaki Mshindo  FC .
Joel Msiba  ni msemaji  wa timu ya  polisi  Iringa alisema  kuwa   timu  yake  imejipanga   vema  kuifunga   timu ya  Mshindo  FC  katika mchezo  wao  huo  utakaopigwa  siku ya jumamosi  huku akiomba mashabiki   zaidi  kujitokeza kushuhudia  mchezo  huo .
Msiba  alisema  kwa  kawaida   timu ya  polisi  ni timu ya  wastarabu  ambao  wapo  kuona  michezo  ndani ya  mkoa  wa Iringa  inahamasishwa na kupitia mashindano hayo  kuhakikisha timu  yake haishiriki  tu bali  inatwaa ubingwa wa mashindano hayo .
Kuanzishwa  kwa mashindano  hayo ya  hayo  ya   kombe la  mbunge Ritta Kabati  kumeendelea   kuhamasisha  vijana  wengi  kushiriki katika  michezo hiyo  ambayo  ilianza kwa  kuwa na  timu zaidi ya  42  na kufanya  mashindano  hayo  kuwa moja kati  ya mashindano makubwa  zaidi kwa  kushirikisha  timu  nyingi  ukilinganisha  na ligi  kuu ya VPL .0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE