Rex Tillerson
Marekani inasema itaziwekea vikwaza nchi ambazo zinafanya biashara haramu na Korea Kaskazini, kwa mujibu wa waziri wa mashuri ya nchi za kigeni Rex Tillerson
Alisema kuwa Ikulu ya White House hivi karibuni itaamua ikiwa itaziwekea vikwazo nchi hizo.Utawala wa Trump umeamua kuiwekea shinikizo zaidi Korea Kaskazini kufuatia na mpango wake wa nuklia.
Majaribio ya makombora ya hivi karibuni ya Korea Kaskazini ambayo yamepigwa marufuku naa Umoja wa Mataifa yamezua shutuma za kimataifa.
Korea Kaskazini inaaminiwa kupiga hatua katika kuunda makombora ya masafa marefu yenye uwezo wa kufika nchini Marekani.

Marekani haina uhusiano wa kibiashara na Korea Kaskazini na imekuwa ikitoa vitisho vya kuyawekea vikwazo mataifa ambayo yanafanya biashara na taifa hilo.
Hata hivyo Bwana Tillerso hakuzitaja moja kwa moja nchi hizo.
Alisema kuwa suala la Korea Kaskazini litazungumziwa na China, mshikika mkubwa wa Korea Kaskazini wakati wa mazungumzo wiki ijayo.
0 comments:
Post a Comment
AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE