June 19, 2017

MAKAMU MWENYEKITI WA BAVICHA TAIFA AKAMATWA NA POLISI


Image result for Sosopi  Bavicha

JESHI  la  polisi  mkoa  wa  Iringa  linamshikilia  makamu  mwenyekiti  wa baraza la  vijana  la  chama  cha Demokrasi na maendeleo (BAVICHA ) Taifa  Patrick Ole  Sosopi  kwa  tuhuma za kufanya  mikutano ya  hadhara  bila  kuwa na  kibali  cha  jeshi  la  polisi .

Kaimu kamanda  wa  polisi  mkoa  wa Iringa  John  Kauga ameueleza mtandao  huu wa matukiodaimadaima   kuwa  Sosopi alikamatwa  leo asubuhi na  kuwa bado  jeshi  hilo  linaendelea  kumshikilia kwa mahojiano kabla ya  kufikishwa mahakamani kwa kosa la  kufanya  mikutano  bila  kibali  cha  jeshi hilo kwenye  vijiji viwili  vya  Kinyika  na Mlowa  jimbo la Ismani  wilaya ya  Iringa mkoani  hapa .

Alisema  kuwa  makamu  mwenyekiti  huyo wa Bavicha alipewa kibali  ya  kufanya  mikutano ya  ndani  ambayo  inaruhusiwa ila  hakuweza  kufanya  hivyo na badala yake  kufanya mikutano  ya  nje kinyume na  taratibu  na  kuwa mikutano  hiyo  ilifanyika kati ya tarehe 16 na 17  mwaka  huu .

“ Tunaendelea  kumshikilia  Sosopi  kutokana na kosa la  kuvunja  sheria  kwa  kufanya mikutano ya hadhara  pasipo  kuwa na  kibali  cha  polisi kimsingi  mikutano  yote  ya  hadhara  kwa  vyama  vya siasa ilipigwa  marufuku na  mikutano  inayoruhusiwa na  ile ya  ndani  pekee  ila  yeye  aliomba  kibali  cha  kufanya  mikutano ya  ndani  ila  hakuweza  kufanya  hivyo na badala  yake  alifanya  mikutano ya  hadhara nje “

Hata  hivyo kaimu kamanda huyo hakusema  ni  lini makamu  mwenyekiti  huyo wa BAVICHA  Taifa  atafikishwa mahakamani ,hatua   ya  kukamatwa  kwa  Sosopi  imekuja zikiwa  zimepita  wiki  mbili  toka  aliposhikiliwa na kuachiwa kwa  dhamana   jeshi la  polisi  la  polisi  kwa tuhuma  za  kufanya  mkutano katika  eneo la wachimbaji  wadogo wa  madini ya dhahabu  Kijiji  cha Nyakavangala alikamatwa  kwa  agizo la  mkuu wa wilaya ya  Iringa  Richard  Kasesela  kwa madai  ya  kufanya  mkutano  huo Nyakavangala na  kutoa  maneno ya  uchochezi  kwa  wachimbaji hao


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE