June 16, 2017

MAKATIBU WA CCM WILAYA NA MKOA WA IRINGA WAKUTANA NA WABUNGE DODOMA ....

Wabunge wa CCM mkoa wa Iringa na Makati bu wa CCM mkoa na wilaya wakiwa bungeni Dodoma leo
Mbunge wa Mtama Nappe Nauye akisalimiana na makatibu CCM kutoka wilaya za mkoa wa Iringa
Nappe na mzee wa matukio daima
Katibu msaidizi wa CCM mkoa wa Iringa katikati akiwa na wabunge wa Viti maalum mkoa Rita kabati kushoto na Rose Tweve

Mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto ameiomba  serikali kutozuia wananchi kutolima maneo oevu maarufu kama vinyungu.

Mbunge huyo amesema hayo leo bungeni Dodoma wakati akichangia bajeti ya wizara ya fedha na mipango.

Alisema kuwa kuwazuia wananchi kulima vinyungu ni kuwataka Kuwaua njaa.

Alisema kuwa wananchi hao wanategemea kilimo hicho zaidi hivyo ni vema wanaotakiwa kuzuiwa ni wale wanaolima kwenye vyanzo vya maji na sio katika mapito ya maji.

Pamoja na mbunge Mwamoto pia wabunge wote wa mkoa wa Iringa na makatibu wa CCM wilaya zote wakiongozwa na katibu wa CCM Mkoa wamekutana Dodoma pamoja na mambo mengine wamekubaliana kumwita waziri wa Mazingira kufika mkoani Iringa ili kufanya mikutano na wananchi.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE