June 10, 2017

MAJAMBAZI YAVAMIA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI IRINGA ,WAJERUHI WAPORA PESA


Kamanda  wa  polisi  wa  mkoa wa Iringa  Julius Mjengi 
Mkuu  wa  wilaya ya  Iringa  Richard Kasesela  akizungumza na  wanahabari leo 

Baadhi ya majeruhi  waliolazwa  katika Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa wa Iringa  


Baadhi ya  wachimbaji  wadogo  wadogo wa machimbo ya Nyakavangala  Iringa
Na MatukiodaimaBlog
WATU wanaodhaniwa   kuwa  ni majambazi  wamewavamia  wachimbaji  wadogo wa  madini katika  machimbo ya  Nyakavangala  wilaya  ya Iringa  mkoani  Iringa  usiku  wa  kuamkia leo na  kuwapora  pesa  kabla ya  kuwajeruhi kwa  mapanga .

kamanda  wa  polisi  mkoa  wa  Iringa  Julius Mjengi   alisema  kuwa  jumla  ya  majeruhi watano  kati ya  9  ndio  waliolazwa  katika  Hospitali ya Rufaa ya  mkoa wa  Iringa  alisema  kuwa  tukio  hilo limetokea  majira  ya  saa mbili  kasoro  usiku wa kuamakia jana  .

Kuwa  eneo   hilo ni eneo la  wachimbaji  wadogo  wadogo  wa  madini ya  dhahabu  ambalo  lipo  kijiji  hicho  cha Nyakavangala tarafa ya  Ismani  wilaya ya  Iringa .


Hata  hivyo  alisema  msako  mkali  unaendelea  kufanyika  ndani ya mkoa wa Iringa  ili  kuwakamata  wote  waliohusika na tukio   hilo na  kuwaomba  wananchi  kuendelea  kutoa  ushirikiano  katika  kuwafichua  watu hao .


Wakizungumza na  mtandao  wa matukiodaima leo  katika Hospitali ya  rufaa ya  mkoa wa  Iringa  ambako  wamelazwa  hao  walisema  kuwa  watu hao  ambao  idadi yao  inafikia  9  waliwavamia  majira ya saa 2  usiku  wa jana na  kuwataka  watoe  pesa na  wale  waliokaidi  walicharangwa  mapanga  na  kupigwa  na  nyundo  miguuni .

Walisema  kuwa  majambazi hao  walifika  eneo  hilo la machimbo  kwa  kutumia  gari  moja ambayo  haikufahamika na baada ya  kufanya  uporaji  huo  walitoweka  kusiko  julikana .

Alisema  kuwa  majambazi hao  walipora  pesa  kiasi cha  Shilingi milioni 81,950,000 na dhahabu Gram 480 pamoja na  simu 4 kutoka kwa wafanyabiashara  na wachimbaji wa madini  hao  .

Majeruhi katika  tukio  hilo  ni  Mkinya Paulo  (38) mkazi wa Morogoro, Sungari Shija (24) mkazi wa Geita , Bakari  Beka , Fadhili Nalinga  Ramadhani  Mkazi wa  Morogoro, Nsurwa Msanga (30) mkazi wa Bariadi ,Odrick Michael (33) mkazi wa Tanga , Daniel Masanjo (40) mkazi wa  Simiyu na Elia  Benjamini (26) mkazi wa Moshi .

Mkuu wilaya ya  Iringa  Richard  Kasesela   alisema  kuwa  tayari  wilaya  imeweka  ulinzi mkali  pamoja na  kuendesha  zoezi la  utambulisho  kwa  wachimbaji  wote  ili  waweze  kufahamika  na  kuwataka  wachimbaji hao  kuanza  ujenzi wa  kituo  cha  polisi  ili  kuwekewa  polisi eneo  hilo .


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE