June 28, 2017

MAALIM SEIF- HAKI YA WAZANZIBAR INAKUJA BAADA YA MIEZI MIWILI


 Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif amesema haki ya Wazanzibari iliyopotea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 itapatikana ndani ya miezi mitatu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo (Juni 28), Maalim Seif amesisitiza kuwa haki hiyo ipo njiani na haitazidi miezi mitatu itakuwa ishapatikana.
Ameeleza hayo baada ya kuwepo maswali mengi kutokana na kauli zake kuwa atakuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pindi haki yake itakaporejeshwa.
"Haki inakuja si muda mrefu, sina wasiwasi kabisa japo siwezi kusema tarehe gani ila haitazidi miezi mitatu," amesema Maalim Seif.
Ameeleza kuwa mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba si mwanachama wa CUF kutokana na kujivua nafasi yake ya uenyekiti na baraza kuu kuridhia ombi hilo na alipotaka kurejea nafasi yake alitumia nguvu iliyosababisha kuvuliwa uanachama wa CUF.
Maalim Seif amedai kuwa ipo njama ya kusajili wajumbe feki wa bodi ya udhamini ikiwa na malengo manne na hatua mbalimbali zitachukuliwa.
Amefafanua kuwa CUF itafungua kesi dhidi ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita) kwa kosa la kukiuka taratibu za sheria ya wadhamini kwa kutojiridhisha juu ya uhalali wa majina ya bodi ya wadhamini.
"Bodi feki ina malengo makuu manne yafuatayo, kufuta kesi zote zilizofunguliwa, kufungua akaunti mpya benki ili kupata ruzuku, kuwezesha udhibiti wa ofisi za makao makuu Zanzibar na kumuondoa madarakani Katibu Mkuu, Maalim Seif ili kufanikisha njama za kupokonya haki ya Wazanzibari," amesema.0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE