June 27, 2017

LOWASSA AWASILI POLISI KWA MAHOJIANOWAZIRI Mkuu Mstaafu na mgombea urais mwaka 2015 kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa, amewasili katika Makao Makuu ya Polisi jijini Dar saa nne kama alivyotakiwa na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).
Lowassa alikuwa amefuatana na magari manne ya msafara wake pamoja na magari mawili ya polisi wenye siraha.
Kabla ya kuwasili kwa Lowassa, aliyetangulia mapema leo alikuwa katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Mashinji aliyewasili kuhakikisha anaweka sawa maswala ya kisheria na msaada wowote utakaohitajika.
Waandishi wa habari hawakuruhusiwa kusogea eneo la tukio kwani ulinzi umeimalishwa.
Jana Edward Lowassa alipokea wito wa kumtaka aonane na DCI leo saa nne bila kukosa.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE