June 20, 2017

LEO NI SIKU YA WAKIMBIZI DUNIANI


mediaWakimbizi wa Sudan Kusini wanaoishi nchini UgandaREUTERS/Stringer/File photo
Umoja wa Mataifa unasema idadi kubwa ya wakimbizi duniani imeongezeka na kufikia  Milioni 65.6 .
Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia wakimbizi inasema hili ni ongezeko la wakimbizi 300,000 ongezeko lililoshuhudiwa mwaka 2016.
Mkuu wa Tume hiyo Filippo Grandi amesema inasikitisha kuona idadi ya wakimbizi ikiendelea kuongezeka duniani kila wakati.
“Dunia inaonekana kushindwa kulinda amani,” amesema Bwana Grandi.

Aidha, amesema  asilimia 84 ya wakimbizi hao wanaishi katika mazingira magumu na ya umaskini.
Maeneo yaliyo na wakimbizi wengi ni kutoka barani Afrika, Mashariki ya Kati na barani Asia.
Nchi wanazotokea idadi kubwa ya wakimbizi:
  • Syria: Zaidi ya Milioni 5.5
  • Afghanistan: Milioni 2.5
  • Sudan Kusini: Milioni 1.4
Mataifa yepi yanaongoza kuwapa hifadhi wakimbizi ?
  • Uturuki : Milioni 2.9
  • Pakistan: Milioni 1.4
  • Lebanon: Milioni 1
  • Iran: 979,4000
  • Uganda: 940,800
  • Ethiopia: 791,600

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE