June 22, 2017

KKKT DAYOSISI YA IRINGA WAMPONGEZA JPM, ASKOFU MTEULE KUWEKWA WAKFU JUMAPILI

Katibu mkuu KKKT dayosisi ya Iringa Be Nayman chavala akizungumza na wanahabari 
KANISA la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT)  dayosisi ya Iringa limesema maandalizi ya kumwingiza kazini askofu mteule litafanyika jumapili huku likimpongeza Rais Dkt John Magufuli kwa utendaji kazi. 

Katibu mkuu wa KKKT dayosisi ya Iringa Nayman Chavala ameyasema hayo leo wakati akitoa taarifa Kwa wanahabari kuhusu maandalizi yaliyofikiwa ya sherehe kubwa ya  kuwekwa wakfu  kwa askofu mteule Mchungaji Blaston Gavile na msaidizi wake Mchungaji Himidi Saga. 


Alisema   kuwa sherehe ya  kumuingiza  kazini  askofu  mchungaji  Gavile na  msaidizi  wake  Saga  itafanyika   jumapili ya  june 25 mwaka  huu majira ya  saa 3  asubuhi  kwenye  viwanja vya  shule ya msingi  Gangilonga  .

Kuwa  ibada  hiyo  itaongozwa na  askofu  mkuu wa KKKT Dkt  Frederick Shoo pamoja  na askofu  mstaafu Dkt  Owdenburg Mdegella na  kuwa  kabla ya  idaba  kutakuwa na maandamano  ya  wachungaji na  washarika yatakayoanzia usharika wa kanisa kuu hadi  Gangilonga.

" Tunaomba  wananchi  wote na  washarika  kujitokeza kwa  wingi  kushuhudia tukio  hilo la  kihistoria pia  tunategemea  kuwa na viongozi mbali mbali wa  serikali na  wageni  mashuhuri  kutoka ndani na nje ya  Tanzania"

Chavala  alisema  maandalizi  yote  yamekamilika   kwa  ajili ya  tukio   hilo  kubwa  ambalo  lilikuwa  likisubiliwa  kwa  shauku  kubwa .

Askofu  Gavile  amechukua  nafasi ya  aliyekuwa askofu wa kanisa  hilo Dkt  Mdegella ambaye  alistaafu kwa  heshima  kubwa na  kuacha  heshima  ya aina yake  ndani ya KKKT .

Wakati  huo  huo Katibu   huyo  amempongeza Rais  Dkt  Magufuli  kwa  kazi  kubwa  anayoendelea  kuifanya ya  kuwatumikia  watanzania  kwa uadilifu  mkubwa  na  kuwa kazi  kubwa kwa  watanzania  ni  kuendelea  kumpa  ushirikiano .

Kwani  alisema   kuwa  hatua  ya  kuwabana  wasio  waadilifu pamoja na  kupambana na wizi wa mchanga  wa  dhahabu (MAKINIKIA)  ni hatua ya  kupongezwa  kwani suala   hilo  lilikuwa  likiwanufaisha  wachache   huku  Taifa  likibaki  patupu .

" Sisi  kama kanisa  tumekuwa  tukimuombea  kila wakati  tena kwa  kumtaja  kwa  jina na hatutachoka   kuendelea  kumuombea  maana kazi anayoifanya  ni ngumu ambayo silaha  kubwa ni maombi "

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE