June 22, 2017

KIPINDU PINDU CHABISHA HODI IRINGA WAWILI WAPOTEZAMAISHA ,

Mkuu  wa mkoa wa  Iringa Amina Masenza akitoa taarifa ya  ugonjwa wa  kipindu pindu 
Mkuu  wa   mkoa  wa Iringa akitoa taarifa ya ugonjwa wa  kipindupindu 
Mkuu  wa  wilaya ya  Iringa  Richard Kasesela  kulia  akifuatilia  taarifa ya Kipindupindu


SERIKALI  ya  mkoa  wa  Iringa imewataka  wananchi  wa  tarfa ya  Pawaga  wilaya ya  Iringa   kuchukua taahadhali   ya ugonjwa  wa  kipundupindu baada  ya  watu   wawili  kufariki   dunia   wakiwa kwa mganga  wa  kienyeji wakipatiwa matibabu   ya  ugonjwa  huo.


Akizungumza  leo na  wanahabari  ofisini  kwake mkuu  wa  mkoa wa  Iringa  Amina Msenza  alisema  kuwa  ugonjwa  huo  umelipuka  kuanzia tarehe  19 mwaka huu na kuwa  tayari  jeshi la  polisi  linamshikilia  mganga  wa  kienyeji  aliyesababisha  vifo  vya  watu hao wawili .


Alisema  kuwa hadi  sasa wagonjwa 20  wanpatiwa matibabu  na  kuwa  tayari  serikali  imechukua tahadhali  juu  ya ugonjwa   huo .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE