June 1, 2017

KESI YA JESCA MSAMBATAVANGU YAPIGWA KALENDA ,MAHAKAMANI YAAGIZA UPELELEZI UKAMILIKE HARAKA

                                       Jesca  Msambatavangu 

............................................................................................................
                              Na MatukiodaimaBlog 
MAHAKAMA  ya Hakimu Mfawidhi mkoa  wa  Iringa   kwa  imeamuru upelelezi  wa kesi kesi jinai namba 65 ya mwaka  2017 ya aliyekuwa mwenyekiti  wa CCM mkoa  wa Iringa  Jesca Msambatavangu (41) kukamilishwa haraka.
 Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoa wa Iringa David Ngunyale aliuagiza upande wa Jamhuri  kukamilisha upelelezi wa  kesi  hiyo  ili isikilizwe kwa  wakati .

Hakimu  Ngunyale  ameahirisha  leo kesi hiyo  hadi June 26 mwaka huu kesi  hiyo  itafika tena  mahakamani  hapo   huku Msambatavangu akiendelea  kuwa nje kwa dhamana  yake aliyowekewa siku ya kwanza  mahakamani  hapo .

Kutokana na shitaka lililosomwa na mwanasheria   jamhuri Jamhuri Alex  Mwita  mei 2  mwaka huu mahakamani hapo  kuwa Msambatavangu anadaiwa kumshambulia Neema Nyongole mkazi  wa Kibwabwa  katika Manispaa ya  Iringa Februari 17 mwaka huu  katika  eneo la Kibwabwa tukio ambalo ni kinyume na  kifungu  cha  seria kanuni ya  adhabu sura namba 16 marejeo  mwaka 2002.


Dk. Msambatavangu  anayetetewa na mawakili  wawili  Alfred Mwakingwe na Jackson Chaula  katika  kesi  hiyo ambayo kwa siku jana  idadi ya watu waliofika mahakamani hapo  kusikliza ilikuwa ni kama  watu 15 pekee ambao nio rafiki na ndugu zake tofauti na awali ambapo mahakamani hiyo  ilifurika viongozi wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema)

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE