June 28, 2017

KESI YA HALIMA MDEE DHIDI YA SPIKA NDUGAI YAHAIRISHWA

Kesi iliyofunguliwa na wabunge wa CHADEMA akiwepo Mhe. Halima Mdee, John Mnyika pamoja na Ester Bulaya dhidi ya spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai imeahirishwa leo mpaka Juni 29, 2017 ambapo itasomwa tena. 
Wabunge hao wa CHADEMA walifungua kesi hiyo kupinga adhabu walizopewa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kutohudhuria vikao vya Bunge ambapo wabunge Halima Mdee pamoja na Ester Bulaya kwa pamoja wao waliadhibiwa kutohudhuria vikao vilivyobaki vya Bunge la saba pamoja na vikao vyote vya Bunge la 8 na Bunge la tisa huku Mbunge John Mnyika yeye aliadhibiwa kutohudhuria vikao 7 vya Bunge kwa kosa la kudharau mamlaka ya spika.
Mbunge Ester Bulaya pamoja na Halima Mdee wanapaswa kurudi Bungeni mwaka 2018 katika vikao vya Bunge la Bajeti baada ya Kamati ya Haki, Maadili, na Madaraka ya Bunge kuwakuta wabunge hao na hatia ya kudharau Mamlaka ya Spika wa Bunge jambo ambalo wao wanalipinga kwa kufungua kesi.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE