June 14, 2017

JENGO REFU LA MAKAZI LONDON LATEKETEA KWA MOTO

                                     Idara ya wazima moto jijini London imetuma malori 40 ya kuzima moto huo
Jengo moja la ghorofa limeshika moto katika barabara ya Latimer, magharibi mwa jiji la London, watu walio shuhudia tukio hilo wanasema,moto huo umeleta mshituko mkubwa hali iliyosababisha baadhi ya watu kushindwa kutoka katika makazi yao.
Taarifa zinadai kuwa baadhi ya watu bado wamekwama ndani ya jengo hilo linalo waka moto.
Moto huo katika jengo la Grenfell Tower ulianza mwendo wa saa 01:16, saa za Uingereza na karibu wazima 200 wanapambana nao.
Hadi sasa moto huo unaendelea kuunguza jengo hilo vikosi vya uokoaji na zima moto takriban 200 vikiendelea na kazi hiyo.

Idara ya wazima moto jijini London imetuma malori 40 ya kuzima moto huo
Polisi wanamesema kuwa hadi sasa imebainika kuwa ni watu wawili tu ambao wameathirika na moshi wa moto huo na wanapata matibabu huku idadi ya waliokwama ndani ya jengo hilo ikiwa haijulikani. .

Mwandishi wa BBC Andy Moore aliyepo katika eneo la tukio kwa sasa anasema jengo hilo lina wasiwasi wa kuanguka wakati wowote.
Image caption takribani wazima moto 200 wanapambana nao.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE