June 26, 2017

HUYU NDIO MFANYABIASHARA ALIYEFUMANIWA NA MWANAFUNZI IRINGA

Mfanyabiashara  aliyefumaniwa  na mwanafunzi  akiwa katika chumba  cha mwanafunzi  huyo nyumbani kwa  wazazi  wake ,picha ya  mwanafunzi imefunikwa  uso kwa  kuzingatia maadili ya habari.
...........................................................................................................................................................
Na matukiodaimaBlog
AMA  kweli  za  mwizi  arobaini  mfanyabiashara  wa  kitimoto  eneo la  Kihesa  Kilolo  mjini  Iringa Katito  Nganga (35)  afumaniwa na denti  wa  kidato  cha  kwanza  katika  shule  ya  sekondari  Mtwivila (jina tunalo) akivunja  amri  ya  sita .
 
Hatua  ya  kukamatwa  kwa  njemba   hilo imekuja   huku  serikali ikiwa  imetoa onyo  kwa mwanaume ambae atakutwa na  mwanafunzi katika maeneo  tata ama  wakifanya   mapenzi  kukamatwa na  kufikishwa mahakamani na adhabu  yake  ni  jela  miaka  30.

Mashuhuda  wa   tukio  hilo  walimweleza  mwandishi  wa matukiodaimaBlog   kuwa mfanyabiashara   huyo mpenda  madenti  alikutwa na mkasa  huo  juzi  majira ya  saa 5  usiku  akiwa  ndani ya  chumba cha  mwanafunzi huyo  nyumbani  kwa  wazazi  wake  akiendelea kuvunja  amri ya  sita bila  hofu  yoyote .

Imedaiwa  kuwa  imekuwa ni kawaida ya  mfanyabiashara   huyo wa  nyama  ya  kitimoto  kumdanganya  denti  huyo kwa  nyama  na  hata  kumuhadaha  kuwa angemuoa na  kuwa  mke  wake  wa  pili na  kuuza  klabu  cha  pombe  za  kienyeji  cha babake kabla ya  kumtorosha  denti  huyo.

" Tuliweka  mtego  baada ya  kuona nyendo  za  mwanafunzi  huyo  si  zenyewe  na  siku  hiyo  kama  kawaida  yake  mfanyabiashara   huyo  aliingia  chumbani  kwa mwanafunzi  na  kuendelea na mambo  yake  ya  kufanya mapenzi na mwanafunzi huyo ndipo  tulipoita  polisi na kumkamata"

Kaimu  kamanda wa  polisi  mkoa wa Iringa  John Kauga  alithibitisha  kutokea kwa  tukio  hilo  na kuwa mtuhumiwa  huyo  bado anashikiliwa na  polisi  kwa  upelelezi  zaidi kabla ya  kufikishwa mahakamani .

Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Amina  Masenza amewataka  wananchi  mkoani hapa  kuendelea  kutoa  taarifa  ofisini  kwake iwapo  wanataarifa  za  wanaume  wanaojihusisha  urafiki  wa  kimapenzi na  wanafunzi pamoja na wale  wanaobaka  watoto .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE