June 20, 2017

HILI NDILO AZIMIO LA PAMOJA KUHUSU KUPIGWA NA KUDHALILISHWA KWA WATU WENYE WALEMAVU TANZANIA


Wawakilishi wa Asasi za Kiraia zipatazo 35 zinazojihusisha na utetezi wa haki za binadamu kwa Watu Wenye Ulemavu tunaokutana hapa mjini Morogoro kushiriki semina iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) tunalaani vikali kitendo haramu cha Polisi kuwapiga watu wenye ulemavu mnamo tarehe 16/06/2017 wakati wakielekea kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kupata majibu ya maombi yao kuhusu maegesho ya vifaa vyao vya usafiri wanapokua katika shughuli zao za kiuchumi jijini Dar es Salaam.

Aidha Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye Ualbino Tanzania Mkoa wa Mwanza ndugu Alfred Kapole amesema kupigwa na kuteswa kwa watu wenye ulemavu mkoa wa Dar es Salaam si tu kwamba umekiuka Katiba ya Nchi bali pia unakinzana na sheria na taratibu za ukamataji au utulizaji wa ghasia. “Suala kama hili halijawahi kutokea polisi kutumia nguvu kubwa hivi kwa watu wenye ulemavu, mimi sijawahi kushughudia.” Alisema Kapole kwa masikitiko makubwa. Alisema nguvu iliyotumiwa na polisi ilikuwa kubwa mno ukilinganisha na watu polisi waliokuwa wanadeal nao. Hivi polisi anapompiga mtu mwenye ulemavu kwa bomu ya machozi anategemea akimbie kwa kutumia wheel chair?

Wakizungumzia vitendo hivyo vya Polisi, kwa pamoja Stela Jailos kutoka Sauti ya Wanawake Wenye Ulemavu Tanzania na John Mlaba Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Tanzania (CHAWATA) wameitaka serikali kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya Polisi wote waliohusika katika vitendo hivyo haramu.

Walichokifanya polisi ni kuwadhalilisha na kutweza utu wa watu wenye ulemavu. Walichokifanya hakikubaliki kwa mujibu wa Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania pamoja na sheria zingine za nchi ikiwemo sheria ya watu wenye uleamavu ya mwaka 2010. Hatua stahiki lazima zichukuliwe dhidi ya wahusika wa vitendo walivyofanyiwa watu wenye ulemavu mkoa wa Dar es Salaam. Alisema Wakili Novat Rukwago

Kwa upande wake Wakili Gideon Mandesi amewaasa watu wenye ulemavu kudai haki zao zilizovunjwa mahakamani kwa kesi ya Kikatiba kwakuwa wanazo sababu za msingi za kufanya hivyo. Amesema atawasaidia wohanga wote wa kupigwa na kuteswa kuhakikisha wanapata haki zao. Gedeon Madesi.

Aidha tumepokea taarifa kwamba leo wakati Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Mwigulu Nchemba akijibu swali la Mh Stella Ikupa Mbunge wa Viti Maalum amekubali kwamba Polisi walitumia Nguvu kubwa walipokua watu wasio stahilli nguvu hiyo kutokana na hali yao ya ulemavu. Tunamshukuru Waziri kwa kukubali kuwa Polisi walitumia nguvu kubwa kupita kiasi. Lakini haitakua na maana yoyote kama hatua madhubuti za kisheria hazitachukuliwa dhidi ya wahusika. Kwa ujumla majibu ya Waziri hayajitoshelezi na yanamapungufu yafuatayo:
Waziri hajasema ni kwa namna gani atawashughulikia Watu waliohusika na vitendo hivyo.

Waziri ameshindwa kuonyesha ni kwa jinsi gani atawasaidia watu walioathirika na vitendo hivyo viovu kama kujeruhiwa na uharibifu wa vifaa vyao.

Waziri hajasema wale walioumizwa watasaidiwaje kupata matibabu na kurudi katika hali ya kawaida.

Waziri ameshindwa kueleza ni kwa jinsi gani atashughulikia madai ya awali ya walemavu wakwenda kudai kwa Mkurugenzi.

Waziri ameshindwa kutoa amri kwa Jeshi la Polisi kutoa Fomu namba 3 ya polisi kwa wahanga wa tukio hilo ili waweze kutibiwa.
Waziri ameshindwa kupinga kauli iliyotolewa leo na Kaimu Kamanda wa Kanda Malalum ya Dar es Salaam  iliyoendelea kusisitiza kuwa walichofanya polisi  ni sawa.

MAAZIMIO YETU
Sisi Mashirika takriban 35 ya utetezi wa haki za watu wenye ulemavu Tanzania Bara na Visiwani, pamoja na Asasi 10 zinazotetea haki za makundi ndani ya jamii ya watu wenye ulemavu Tanzania tunaazimia yafuatayo;

Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani ichukue hatua kali za kisheria dhidi ya watu wote waliohusika na vitendo hivyo visivyokubalika katika jamii yetu ya Tanzania.

Asasi za Kiraia zinazojihusisha na utetezi wa haki za binadamu kwa watu wenye ulemavu na watetezi wa haki za binadamu kwa ujumla tuungane pamoja kukemea vitendo hivi vya unyanyasaji na udhalilishaji vinavyofanywa dhidi ya watu wenye ulemavu.

Asasi za Kiraia Zinazojihusisha na Utetezi wa wa Haki za Binadamu kwa Watu Wenye Ulemavu zifungue Kesi ya Kikatiba kwenye mahakama stahiki ili kuhakikisha kuwa wahusika wa vitendo hivyo wanachukuliwa hatua zinazostahili.

Asasi za Kiraia zifikishe malalamiko kwenye vyombo vya Haki za Binadamu vya Kimataifa ikiwemo Tume ya Haki za Binadamu ya Africa na Baraza la Haki za Binadamu za Umoja wa Africa.

Asasi za Kiraia zinazotetea haki za watu wenye ulemavu zinamwomba Mhe Rais aingilie kati suala hili na  kuwataka watumishi wake waheshimu haki za watu wenye ulemavu kama zinavyolindwa na katiba pamoja na mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeridhia.

Azimio  hili limetolewa leo tarehe 20 Juni 2017 na Asasi za kiraia zipatazzo 35   zinazojihusisha na utetezi wa Haki za Binadamu kwa Watu wenye Ulemavu tunaohudhuria Warsha ya Mafunzo Kuhusu Mifumo ya Utetezi wa Haki za Binadamu Kikanda na Kimataifa iliyoratibiwa na Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadazmu Tanzania (THRDC) hapa Mjini Morogoro.

Azimio hili limetolewa leo tarehe 20 Juni 2017 na Asasi zifuatazo:


Chama cha Walemavu wa Viungo Tanzania  CHAWATA
Chama cha Viziwi Tanzania CHAVITA
Tanzania Albinism Society TAS
Tanzania League of the Blind  TLB
Tanzania Society of Deaf and Blind  TASODEB
Kilimanjaro Association of Spinal Cord Injuries  KASI

Psoriasis Association of Tanzania PSORATA
Association for Spinal Bifida and Hydrocephalus Tanzania  ASBAHT
Tanzania Users and Survivors of Psychiatric Organisation -TUSPO
Sauti ya Wanawake Wenye Ulemavu Tanzania- SWAUTA
Chama cha Watu Wenye Ualbino Mwanza
Home Start for Disability Organisation (HSDO)
Umoja wa Watu wenye lemavu Zanzibar-UWZ
Under The Same Sun- UTSS
SHIVYAWATA
Zanzibar Centre for Development of Inclusive Disables-ZACDID
Child Wach
Tanzania Society for Blind (TSB)
Tanzania Association of Mental Handicapped (TAMH)
Centre for Disability Empowerment Promotion (CIDEPRO)
Tanzania National Institute for the Blind (TNIB)
Tanzanite Disability Organisation (TADIO)
Tanzania League of the Blind (TLB)
DOLASED
Information
Centre on
Disability
Tunaweza Kituo cha Shughuli Na Msaada wa Ajira kwa Vijana Wenye Ulemavu
Deaf Blind Within the Teachers Forum (DBWITEFO)
Comprehensive Support to Persons With Disabilities (COSUPED)
TASU

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE