June 15, 2017

HIFADHI YA UZUNGWA SCARP YATAKIWA KUHAMASISHA UTALII KILOLO

Mwenyekiti wa kamati ya  ulinzi na usalama wilaya ya  Kilolo  Asia Abdalah  akizungunza  wakati wa  utambulisho wa mradi wa Uzungwa Scarp  leo
Kaimu  meneja  wa Hifadhi ya  Uzungwa Carp Yusiph  Tango  akitambulisha  mradi  wa  uhifadhi wa  misitu ya hifadhi ya Uzungwa Carp  leo mbele ya  wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama  wilaya ya Kilolo
Kaimu  meneja wa hifadhi ya  misitu ya  Uzungwa Scarp Yusuph  Tango  akitambulisho  mradi  wa  uhifadhi wa misitu  katika  hifadhi ya  Uzungwa Scarp  leo 

 Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo  Asia Abdalah   katikati  akiwa na  wajumbe wa  kamati ya  ulinzi na usalama  pamoja na kaimu  meneja  wa hifadhi ya  misitu ya  Uzungwa Scarp  Yusuph  Tango  wa  tano  kulia  mara  baada ya  kutambulisha mradi  wa  Uzungwa Ccarp  wa  kuhifadhi misitu 

Na  MatukiodaimaBlog
SERIKALI ya wilaya ya Kilolo mkoani Iringa imepongeza jitihada zinazofanywa na mradi wa Uzungwa Scarp katika kuhifadhi na kuhamasisha utalii ktika hifadhi hiyo na kutaka kasi ya uhamasishaji wa utalii izidi kutolewa.

Akizungumza wakati wa utambulisho wa mradi wa Uzungwa Scarp  leo   ,Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah alisema kuwa jitihada za serikali ya wilaya hiyo ni kuona lango  la utalii katika wilaya ya Kilolo linafunguliwa ili  kuwezesha wananchi wa wilaya hiyo kukuza uchumi wao.

Alisema kuwa wilaya ya Kilolo yenye hifadhi zaidi ya moja ikiwemo hifadhi ya misitu ya Uzungwa Scarp na ile ya Hifadhi ya Taifa ya misitu ya Udzungwa ila bado kasi ya utalii inaweza kuongezeka na kuwa na maslahi zaidi kwa wananchi.

Mkuu huyo  wa wilaya alisema kuwa moja kati ya mipango ya serikali ya awamu ya tano  chini ya Rais Dkt John Magufuli ni kuona Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda na kupitia utalii kuna  uwezekano viwanda zaidi kuanzishwa Kilolo.

Hata hivyo  aliagiza hifadhi ya Mistu ya Uzungwa Scarp kuandaa eneo la kuwagawia wawekezaji kwa ajili ya ujenzi wa Hoteli  za kitalii badala ya kuendelea kuhamasisha utalii bila kuwa na hoteli  za watalii kufikia.

Aidha alisema ili  uhifadhi huo uwepo ni lazima suala la uharibifu wa mazingira kusimamiwa kwa kuona moto hauharibu mazingira ya hifadhi hiyo.

Hivyo alisema serikali ya wilaya itahakikisha inatoa ushirikiano mkubwa kwa hifadhi hiyo na nyingine ili  kuhakikisha wananchi hawaharibu mazingira ovyo ama kuingia ndani ya hifadhi hiyo.


Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilolo Vallence Kihwaga pamoja na kupongeza hifadhi hiyo na wahisani wa UNDP kujitolea kujenga daraja la kuunganisha kijiji cha Uluti bado alitaka wananchi kutafutiwa shughuli nyingine kama za ufugaji wa samaki ili  kupunguza kasi ya uwindaji hifadhini.

Alisema iwapo wananchi wataanzishiwa miradi ya ufugaji wa samaki ama mifugo mingine wataacha kuingia hifadhini  kuwinda wanyama.

Kaimu mhifadhi wa hifadhi ya Uzungwa Scarp Yusuph Tango alisema kuwa hifadhi hiyo kijografia ipo Kilolo ,Mufindi na Kilombero  na kwa Kilolo ina vijiji 7 na jumla ya vijiji vyote kwa Kilolo,Mufindi na  Kilombero vinavyo pakana na hifadhi ni  19 na vyote vinanufaika na hifadhi hiyo kwa kusaidiwa shughuli mbali mbali za kimaendeleo.

Alitaja fursa zilizopo kuwa ni utalii na utafiti,ajira,uwekezaji kama Hoteli, Ufungaji nyuki,uzalishaji wa maji ya kunywa na nyingine nyingi.

Hata hivyo alisema changamoto kubwa ni uwindaji na utegaji wa wanyama ndani ya hifadhi,ukataji miti ndani ya hifadhi kwa ajili ya mbao ,kuni,nguzo na mkaa.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE