June 29, 2017

DR MAGUFULI AMLILIA DR TONIA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Joseph Pombe Magufuli amesema amepokea kwa mshtuko mkubwa kifo cha Mkurugenzi Mkuu wa benki ya AFDB Dkt Tonia Kandiero kilichotokea usiku wa jana, na kusema kwamba ni mtu aliyechangia maendeleo Tanzania.
Rais Magufuli akiwa na Dkt. Tonia enzi za uhai wake.
Rais Magufuli ametuma salamu hizo za rambirambi kwa Rais wa benki hiyo Akinwumi Adesina na kusema kuwa Dkt Tonia atamkumbuka kama hodari na mchapakazi katika kipindi cha uhai wake na kwamba kwa kushirikiana kwao kulifanikisha kukamilika kwa miradi mikubwa iliyokuwa chini ya ufadhili wa AFNB.
Kifo cha Dkt Tonia kimetokea usiku wa jana Juni 28 alipokuwa ofisini kwake huko Pretoria Afrika kusini.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE