June 7, 2017

WANAFUNZI SHULE YA SOUTHERN HIGHLANDS MAFINGA WATEMBELEA HIFADHI YA RUAHA KUJIFUNZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Walimu na  wanafunzi wa  shule ya  Msingi ya  Southern  Highlands  Mafinga  mkoani  Iringa  wakitazama moja kati ya  mito  ya  inayoanzia  ndani ya  hifadhi ya  Ruaha ambao  umekauka
Wanafunzi  wa  shule ya  Msingi  Southern Highlands  Mafinga mkoa wa  Iringa wakitazama  jinsi  mto  Ruaha  mkuu  unaopita  ndani ya  hifadhi ya Taifa  ya Ruaha  ulivyoanza  kukauka  kutokana na  uharibifu  mkubwa wa mazingira  unaoendelea  kufanywa na  wananchi  wanaoendesha  shughuli za kilimo kando ya  mto  huo


Jitihada  za  kulinda  mto  Ruaha  mkuu  zinapaswa  kuungwa na mkono na kila mdau  ili  kuufanywa mto  huo  kuendelea  kuwa na maji  msimu wote wa mwaka
Hali  halisi ya  mto  Ruaha  inavyoonekana   sasa  hii  imetokana na uharibifu  mkubwa wa mazingira  unaofanywa katika  mito  mbali mbali  inayoingiza  maji  mto huo 
Kiboko  wakihangaika  kutafuta kina  kirefu  cha maji ndani ya  mto  Ruaha  mkuu  hifadhi ya Taifa ya  Ruaha

Na  MatukiodaimaBlog
KATIKA  kuwawezesha  watoto  kuendelea  kupenda  uhifadhi wa mazingira  katika  maeneo wanayoishi  pia  kuunga  mkono jitihada za  serikali ya  awamu ya tano ya  uhifadhi wa mazingira ,uongozi wa  shule ya msingi ya  Southern Highlands Mafinga  wilaya ya  Mufindi  mkoa  wa  Iringa umewapeleka  wanafunzi  wake  katika  hifadhi ya  Taifa ya  Ruaha  ili  kuona madhara  ya  uharibifu wa mazingira  yalivyochangia  wanyama  kuishi  kwa  shida  katika  hifadhi  hiyo .

Mwalimu kiongozi wa  ziara  hiyo ya  wanafunzi  wa  shule ya  Southern Highlands  Mafinga ,  Abas  Rashid  alisema  kuwa wanafunzi  hao  wa  darasa  la  kwanza na la pili wapatao 50  wamefika  hifadhi hiyo ya  Ruaha  ili  kuweza kujifunza   kwa  vitendo uhifadhi  wa mazingira  pia  kufanya  utalii  wa  ndani  ili  wanafunzi hao  kuoa  uhalisia wa  masomo  ya  mazingira   na  wanyama .

Alisema  kuwa   katika  ziara  hiyo wamepata  kutembelea  maeneo  mbali mbali  ya  hifadhi  hiyo  na kuona  jinsi gani  ambavyo  mto  huo Ruaha  mkuu  unavyoendelea  kupungua maji  na  hivyo bado  jamii  inapaswa  kusaidia  kunusuru  mto  huo .

Rashid  alisema  kuwa shule   hiyo imekuwa na utaratibu wa kuhifadhi  mazingira  yanayozunguka  shule  pamoja na  kuwafundisha  masomo ya  mazingira  na  utalii  wanafunzi  hao  hivyo kufika katika  hifadhi  hiyo ya  Ruaha  ni mwanzo  mwema  wa  kuwawezesha  watoto hao  kupenda  zaidi masomo  hayo na  kuwa  kielelezo  bora  kwa  jamii wanayoishi .


Michael Minja  ni muongoza  watali katika  hifadhi  hiyo  ambaye  aliwaongoza  wanafunzi hao  alisema  kuwa  shughuli  mbali mbali za  kilimo kisichozingatia  uhifadhi wa mazingira katika  eneo la Mbarali  ni  chanzo  cha  mto  huo kuendelea  kukauka .

Hivyo  alisema  ili  mto  huo uzidi  kuwa  salama  lazima  shughuli za  kilimo kisichozingatia  uhifadhi wa mazingira   kuweza kuondolewa wakiwemo  wale wa  bonde  la usanga kwani   maji  yote yakielekezwa  mto  Ruaha  mkuu kuna  uwezekano wa mto  huo  kuongezeka  zaidi .

Alisema  maji  yaliyopo  hadi  mwezi  wa 11 mto  huo  utabaki  kuwa na madimbwi  pekee  hautakuwa na uwezo wa  kutiririsha  maji  tena  kwani  hali  ya  sasa  si nzuri inatishia  mto   huo  kukauka  kabisa .


Ahmed  Nasoro  afisa utalii   na masoko  hifadhi  ya  Ruaha  anasema  kuwa  upo  utaratibu wa  kuwaelekeza  watalii  wanaofika katika  hifadhi   hiyo  ili  pindi  wanapokuwepo  ndani ya  hifadhi  kutunza mazingira .

Pia  aliwataka  watalii  zaidi  kuendelea  kutembelea  hifadhi  hiyo  pamoja na kuungana  kutunza ikolojia  ya  mto  Ruaha  mkuu  hasa kwa  maeneo  ambayo  yanamwaga maji  yake katika  hifadhi  hiyo ya  taifa .


Tayari  shirika  la hifadhi  za Taifa (  TANAPA)  limeanzisha  tuzo ya  utunzaji wa mazingira katika  mikoa ya  Iringa , Njombe na Mbeya  kwa  washindi  kupewa pesa  pamoja na  cheti  cha  kupongezwa kama  sehemu ya  kuhamasisha  wananchi  kutunza  mazingira .

Tuzo   hizo  zimeendelea  kutoa  hamasa  zaidi na  hata  kupelekea  shule  ya  Southern Highlands  Mafinga   kupania  kushiriki mwakani  na  kuwa  imani  yao  kutwaa tuzo  hizo za mazingira .


Tayari  makamu  wa  Rais Samia  Suluhu  Hassan  ameunda  kikosi  kazi cha  kuokoa  ikolojia ya  mto  Ruaha  mkuu ambacho  kimeanza  kazi kama  njia  pekee ya  kulinda  mazingira  ya  mto  Ruaha .
0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE