June 8, 2017

BAJETI HII INA UMA NA KUPULIZIA -WANANCHI IRINGA


Mkazi wa Muwimbi wilaya ya  Iringa akifyatua  tofari  kutafuta  kipato chake
Zen Mkadam  akitoa  maoni yake  kuhusu  bajeti  ya  serikali  iliyosomwa  leo bungeni Dodoma
Mussa Mhema  akitoa maoni yake juu ya bajeti hiyo

Na MatukiodaimaBlog 
WAKATI  leo  bajeti  ya mwaka 2017/2018 imesomwa mjini Dodoma  ,wananchi  mkoani  Iringa wamesema  bajeti  ya  wizara ya  fedha  na mipango  iliyosomwa na   waziri  wa  wizara  hiyo Dkt  Philip Mipango    ni bajeti inayouma na  kupulizia  na kuwa serikali  ilipaswa  kubuni vyanvyo  vipya  vya  kukusanya mapato  badala ya  kufuta  upande mmoja na  kuongeza upande  wa pili .

Zen Mkadam  mkazi wa mjini  Iringa  alisema  kuwa  sehemu  kubwa  hawaja bajeti  hiyo  haina  tofauti na  bajeti  zilizopita  ambazo Sigara  na  vinywaji  vya  vikali  huwa  bei  juu   huku  bidhaa  nyingine  hushushwa bei  kama   maji  ,soda na vinywaji  vinavyotokana na matunda kutoka  ndani kama  Zabibu na matunda  mengine .

“ Mimi  nilitegemea  bajeti  hii ya serikali yaawamu ya  tano  ingempa nywanya  zaidi  mwananchi wa kawaida  na  badala yake  makusanyo ya  serikali  yangetafutiwa vyanzo  vingine kama  bandarini na maeneo  mengine  ambayo kimsingi yanaweza  kusaidia kuendesha  nchi  hii  kimapato “

Mkandam  alisema  kwa upande wake  haungi  mkono  msamaha  uliotolewa  kwa watu  wenye  magari mabovu na  walioegesha  ambao  wamepewa msamaha  na  badala  yake  watakaolipa motor vehicle ni  wale  wenye magari yanayotembea pekee .

Huku Musa  Mhema  ambae  ni  dereva  Taxi  eneo la M.R mjini  Iringa alisema kuwa amependezwa  na bajeti  hiyo hasa  kusikia  Motor Vehicle kwa magari yasiyo tembea  imefutwa pia  punguzo mbali mbali  zilizotolewa  kama  kuondoa ushuru   kwa ujazo  usio zidi  tani  moja kwa usafirishaji wa mazao hayo  ya  chakula .

Pia  alisema  anaipongeza  serikali kwa  kufuta  VAT  kwa vyakula  vya  mifugo  vinavyozalishwa  hapa nchini  kwani  itasaidia  kupunguza  maghara kwa  wafugaji  hapa  nchini .

Yohana  Sanga mkazi wa Ihemi  Iringa  alisema serikali   hatua ya  kuongeza bei ya mafuta  katika  vituo vya mafuta  kutawatesa  wananchi  wanyonge  na  kuwa ilikuwa vema  wale  wote  walioshindwa   kulipa Motovehicle  ambao  wanadaiwa  kulipa madeni yao badala ya  kufuta  kodi hiyo na  kupeleka  vituo vya mafuta .

Ismail  Huwel alisema  kuwa bajeti  hiyo  ambayo  ina ongezeko la  zaidi ya  asilimia  tatu ni  bajeti  nzuri  ambavyo  imetoa unafuu kwa kila mtanzania na  kuwa serikali ya  Rais Dkt John Magufuli  imeonyesha  usikivu  mkubwa kwa  wananchi  wake na kuwa kutokana na bajeti  hiyo  imani ya  watanzania  inazidi  kuongezeka  zaidi.

Alisema  pamoja na bajeti nyingine  kuonyesha  kuwagawa  watanzania ila bajeti hii  imeonyesha  kuwaunganisha  watanzania  wote

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE