May 16, 2017

WAZIRI JAFO AMPONGEZA MBUNGE KABATI KWA KUKARABATI SHULE YA MSINGI AZIMIO

Naibu Waziri ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa Selemani Jafo kulia  akiwa na  mkuu  wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah ,mbunge wa  kilolo Venance Mwamoto , mbunge wa  viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati na  mkurugenzi wa Manispaa ya  Iringa Dkt  Wiliam Mafwele  leo  baada ya kutembelea  shule ya Msingi Azimio ambayo mbunge kabati na diwani wa Mshindo  kwa  kushirikiana  na  wadau  wameikarabati
Waziri Jafo  kushoto  akizungumza na wananchi  pamoja na viogozi Manispaa ya Iringa  kutoka  kulia ni mkurugenzi wa Manispaa Dkt  Wiliam Mafwele  akifuatiwa na diwani wa kata ya Mshindo  Ibrahim Ngwada
Mbunge wa  kilolo Venance  Mwamoto  akisalimiana na mkurugenzi wa Manispaa ya  Iringa Dkt  Wiliam Mafwele  kulia katikati ni naibu  waziri wa Tamisemi Mh  Jafo
Naibu Waziri ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa Selemani Jafo akiwasilia  shule ya Msingi Azimo mjini Iringa  leo kushoto kwake ni mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto
Naibu Waziri ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa Selemani Jafo  akipata  utambulisho  shuleni Azimio
Naibu Waziri ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa Selemani Jafo  akiwa na  viongozi mbali mbali
Naibu Waziri ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa Selemani Jafo  akitembelea  madarasa ya  shule ya Msingi  Azimio  mjini Iringa
Naibu Waziri ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa Selemani Jafo  akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya  wananchi  wanawake  waliofika  shuleni hapo leo
Naibu Waziri ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa Selemani Jafo  akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya  wananchi  wanaume  na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati na mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah aliyemwakilisha mkuu  wa  mkoa katika msafara   huo   katika  ziara  yake shule ya Msingi Azimio  leo
Naibu Waziri ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa Selemani Jafo  akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya  viongozi wa  Manispaa  wilaya na wabunge   waliofika  shuleni hapo leo
Na MatukiodaimaBlog
NAIBU waziri ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa Selemani Jafo  amepongeza jitihada  kubwa za  kimaendeleo  zinazofanywa na mbunge  wa  viti  maalum  mkoa  wa Iringa kupitia  chama  cha mapinduzi (CCM)  Ritta Kabati kwa  kujitolea  kukarabati shule  ya  msingi Azimio iliyopo kata ya Mshindo  kwa  kushirikiana na diwani wa kata  hiyo Ibrahim Ngwada na  kuwa ofisi  yake inapongeza kazi  hiyo.

Akizungumza  leo na  wananchi wa kata ya Mshindo  shuleni  hapo ,Waziri  Jafo  alisema  kuwa  kuwa zipo  changamoto  nyingi  ndani ya Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa  katika   sekta ya  elimu  hasa  uchakavu wa majengo  ya  shule  na  nyingine    na kuwa  ufumbuzi  wake ni  kama  huo  ulioanzishwa na mbunge Kabati chini ya diwani wa kata  hiyo na  wananchi kwa  kujitolea  nguvu  zao .

Hata  hivyo  alisema  kuwa amevutiwa na kazi  iliyofanyika kwenye  shule  hiyo kwa  kukarabati majengo  hayo ambayo  yamejengwa  mwaka  1969  na  yalikuwa katika hali  mbaya  zaidi hivyo   ukarabati huo  umefanya majengo hayo  kuwa katika hali  ya  kuvutia   zaidi .

Waziri Jafo  alisema  kuwa alipata  kufanya  ziara  yake  mkoa  wa Iringa na  kubaini  changamoto  mbali mbali  ndani ya Manispaa ya  Iringa na maeneo  mengine na  kuwa serikali ya  Rais Dkt  John Magufuli imekusudia  kuondoa  changamoto  mbali mbali katika nchi .

Alisema  kuwa  serikali  imejiwekea  mipango  mbali mbali  ya kusukuma maendeleo  ndani ya  mkoa  wa Iringa  japo  ushiriki  wa  wananchi  na  wadau  bado  unahitajika  katika  kuendeleza jitihada za  mbunge Kabati  katika  kukarabati  shule  mbali  mbali za Manispaa ya  Iringa.

“ Kweli nawapongeza  sana  kazi kubwa mnayofanya wananchi wa Iringa na mnaonyesha  wazi  kuwa kweli  wananchi katika mradi wa  kugatua madaraka  kwa wananchi  inayonyesha   wazi wananchi  wanashiriki vema  na kuna haja ya  wabunge  wengine  kuiga mfano  huo  pia nimpongeza  mbunge  wenu Kabati ni mmoja kati ya  wabunge  wanaofanya  vizuri mbali ya kukarabati shule  amejitolea  kujenga kituo  cha  polisi “

Waziri  Jafo  alisema  kuwa  serikali itaendelea  kusaidia mkoa  wa Iringa  ili  kupiga hatua  ya  kimaendeleo na kuwa  wabunge wake  wamekuwa  mfano bungeni kwa  kupiga  kelele  juu ya  maendeleo ya wananchi .

Wakati  huo  huo Jafo  ameahidi  kusaidia  kutoka  vitanda na magodoro  kwa  ajili ya Hospitali ya  Flerimo ambayo ni  Hospitali ya  Manispaa ya  Iringa .

Alisema  kuwa  serikali itaendelea  kuboresha hospitali ya Flerimo na tayari  rais Dkt Magufuli ametoa  pesa  ambazo zimenunua  vifaa  mbali mbali kama  mashuka ,magodoro na vitanda  kwa ajili ya  Hospitali mbali mbali  hapa nchini  ikiwemo ya  Frelimo  na  kuwa  vifaa hivyo  vitafika wakati  wowote .

Mbunge Kabati alisema  kuwa   kuwa  alilazimika  kuanza harakati  za  kukarabati  shule  hiyo ya  Azimio na nyingine za Manispaa ya  Iringa kutokana na shule  hizo  kuwa katika hali mbaya na kuwa  mpango  huo wa ukarabati wa  shule zaidi  za Manispaa ya  Iringa  utaendelea katika  shule za Manispaa ya  Iringa.

Akisoma taarifa  ya   shule  hiyo  mkuu  wa shule  ya  Azimio  Sigfred  Mapunda alisema  kuwa shule  hiyo  yenye  darasa la  awali  hadi darasa la  saba ina wanafunzi 240 na  walimu  11  wakati mahitaji ya nyumba  za  walimu ni 11  zilizopo  ni 9  wakati  vyoo  vyawanafunzi  na  walimu  vipo  vya  kutosha .

Kuwa changamoto  zinazoikabili shule  hiyo ni uzio  wa kuzunguka  shule ,ofisi ya  walimu ,uchakavu wa majengo ,chumba maalum kwa ajili ya wasichana ,pesa  za malipo ya mlinzi wa  shule .

Japo  alisema  kuwa tayari  diwani na mbunge  Kabati  wameanza  kutatua  changamoto  mbali mbali  ikiwemo ya ukarabati  wa  shule  hiyo kupitia  wadau mbali mbali  kama mkuu wa  wilaya ya Iringa  Richard Kasesela,familia ya  Salim Asas , Mkanadarsi Geofrey Mungai , mfanyabiashara  Masiti , Mfanyabiashara  MT  Huwel pamoja na  madiwani  na  wananchi  ambao waliunga mkono kazi hiyo .

Pia  alisema mwezi  machi 2015 ofisi ya mkurugenzi wa Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa  imepata  kutoa pesa kiasi cha shilingi  milioni 10 na  kuwa ili  kukamilisha ukarabati  huo  kiasi  cha shilingi  milioni 26 zinahitajika kukamilisha kazi hiyo.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE