May 24, 2017

WAZAZI NA VIONGOZI WATAKAO POKEA PESA KWA WALIOWAPA MIMBA WANAFUNZI KILOLO KUKIONA

Mkuu wa  wilaya ya  Kilolo  mkoa wa Iringa Asai Abdalah akizungumza na wanafunzi wa kidato cha kwanza  shule ya  sekondari  Ilula leo
Walimu wa  shule ya  sekondari Ilula na  wanahabari  wakiwa katika kikao cha mkuu wa wilaya  ya Kilolo  leo
Na MatukiodaimaBlog
SERIKALI  wilaya ya  Kilolo  mkoani  Iringa  imetangaza  kuwachukulia  hatua kali  wazazi na  viongozi  wa  serikali  za   vijiji na vitongiji aambao  watasaidia kutorosha wanaume  wanaowapa mimba  wanafunzi katika maeneo  yao .
Agizo hilo  limetolewa na mkuu wa  wilaya ya  Kilolo Asia Abdalah  wakati wa ziara  yake ya  kutembelea  shule  za msingi na  sekondari  katika kata ya  Ilula wilayani  humo  leo ,kuwa  imekuwa ni kawaida ya  wazazi  kwa kushirikiana na baadhi ya  viongozi wa serikali za  vijiji na vitongoji  kupokea  pesa  kutoka kwa  wanaume  wanaowapa  mimba  wanafunzi  kasha  kuwatorosha .
Mkuu  huyo wa  wilaya  alisema kuanzia  sasa mzazi ama kiongozi atakayebainika  kushiriki kupokea  pesa au  kumtorosha mtuhumiwa wa mimba   kwa  wanafunzi atakamatwa na kufikishwa mahakamani pasipo  huruma .
Hivyo alitaka  kila mzazi  na  kila mwananchi kuhakikisha  wanakuwa  sehemu ya  ulinzi wa watoto  hao wa kike na pale  inapobainika  kuwa mwanaume ana mahusiano na  wanafunzi kuchukua hatua haraka ya kumfikisha kwenye  vyombo  vya  sheria .
Aidha  alisema kazi ya  viongozi wa  serikali  za  vitongoji na vijiji ni kuwalinda  watoto hao  wa  kike  dhidi ya  wabakaji kwa  kuwakamata na  kuwafikisha  polisi huku wazazi  hawana sababu ya  kukaa chini ya  watuhumiwa hao  wa mimba kwa lengo la  kumalizana nje ya vyombo  vya  sheria .
Asia  alisema anajivunia  kuona wananchi wa  wilaya ya  Kilolo  baadhi yao  wameanza  kuwa  walinzi  wazuri wa  watoto  wa  kike na hata  kushiriki kuwafichua wabakaji na  walawiti dhidi ya  watoto katika maeneo  yao huku  akidai kuwa mfano  mzuri ni  kata ya Ilula  ambayo  imefanikisha  kuwakamata  watuhumiwa  wawili kati ya watano  wa ubakaji wa  wanafunzi na kuwafikisha mahakamani na  wote  wawili  wamefungwa  jela maisha .
Alisema pamoja na  watu hoa  wawili  kufungwa jela maisha  bado  jeshi la polisi  Kilolo linaendelea kuwasaka  watuhumiwa  watatu  wa mimba  za  wanafunzi  ili  kuwafikisha mahakamani .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE