May 17, 2017

WANANCHI KIJIJI CHA KIWALAMO WILAYA YA KILOLO WAPONGEZA SERIKALI KUTENGA PESA ZA DARAJA LAO

Meneja  wa benk ya NMB Kilolo Mary Ngalawa akivuka daraja na viongozi mbali mbali akiwemo mkuuwa  wilaya ya Kilolo Asia Abdalah wa tatu  kulia walipotembelea kijiji  cha Kiwalamo leo
Mkuu  wa wilaya ya  Kilolo Asia Abdalah na kamati ya  ulinzi na usalama wakitembelea daraja la  kijiji  cha Kiwalamo lililokwama kumalizika na kuwa kero kwa  wananchi
Daraja la mto Lukosi  ambalo  wananchi wa kijiji  cha Kiwalamo wanalitumia kwa  shida
wananchi wa  Kilawamo wakiwa katika daraja la  mto Lukosi leo
Dc  Kilolo  akizungumza na wananchi wa kijiji  cha Kiwalamo leo
Mwonekano wa daraja  hilo
Mary  Ngalawa  meneja wa bank ya NMB Kilolo akivuka katika  kivuko cha muda daraja la mto Lukosi leo
Daraja  la mto Lukosi
mkuu  wa wilaya  ya Kilolo Asia Abdalah akivuka daraja la  mto  Lukosi ambalo serikali  imetenga milioni 239 kwa ajili  ya ujenzi wa daraja  hilo

Mwakilishi wa meneja  wa wakala  wa barabara mkoa wa  Iringa akikagua daraja la mto Lukosi
Na Matukiodaima BLOG
WANANCHI  wa   kijiji  cha  Kilawamo wilaya  ya  Kilolo  mkoani Iringa  wameipongeza serikali kwa  kutenga  kiasi cha  shilingi  milioni 239  kwa  ajili ya  kuwajengea daraja  la mto Lukosi ambalo  limekuwa  ni kero  kubwa  kwao  kuvusha  wagonjwa .

Wakizungumza  katika mkutano  wa  hadhara  wa  mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo  Asia Abdalah  aliyefanya ziara  katika kijiji  hicho leo na kukagua daraja  hilo , wananchi  hao  walisema  kuwa  wamekuwa wakipata  shida  kubwa  sana  kuvusha  wagonjwa kwa machela katika daraja  hilo  ambalo ujenzi  wake  ulikwama kuendelea  kwa  zaidi ya  miaka mitano  sasa.

Hivyo  walisema  kutokana na kutokamilika kwa  daraja hilo  wananchi wa Kiwalamo  walilazimika  kujitolea kuanza  ujenzi wa daraja  la muda  kwa ajili ya kupata daraja  ya  kuwavusha katika mto  huo mkubwa ila  hata  hivyo bado nguvu yao imekuwa  ndogo kukamilisha daraja  hilo la muda na  wameishia  kutandika miti pekee alisema  Jesca Mlaki .

Kuwa wananchi hao  walianza kujenga  daraja  la kwao la muda ambalo baadae lilivunjwa na  wataalam  wa wilaya ya  Kilolo kwa  ajili ya kuanza ujenzi wa daraja  la kisasa  ambalo hata  hivyo  lilikwama kuendelea baada ya mkandarasi  wa kazi  hiyo  kutoonekana akiendelea na  ujenzi  huo .

Alisema kuwa  wao wananchi  wapo  tayari  kuendelea kutoa  ushirikiano kwa kujenga  kivuko cha muda kwa ajili ya kusaidia  kuvusha  wagonjwa na wananchi kupata  kuvuka katika  mto huo japo  wanaomba serikali  kuweza kuwaongeza  nguvu wananchi  watakaojitolea  kujenga kivuko  hicho  cha muda .

Wakati Ajuaye Kilave  alisema  kuwa  serikali inapaswa  kuwaunga mkono  kwa  kusaidia baadhi ya  pesa kwa  ajili ya kusaidia  ujenzi wa kivuko  cha muda katika eneo hilo kwa  ajili ya kukodi  trekta  na  kupata  pesa  za kununua nguzo   za  kujengea  daraja  hilo .

Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo Asia Abdalah alisema  kuwa  serikali itawaunga  mkono katika  ujenzi  wa kivuko   hicho  cha muda ikiwa ni pamoja na  kuwaleta  wataalam kutoka  Halmashauri na Tanroads mkoa  wa Iringa  kwa  ajili ya  kusimamia  zoezi hilo pia  kuwawezesha  wananchi wanaojitolea  kupata huduma ya  chakula  pindi  wanapofanya kazi  hiyo .

Kwani  alisema tayari  vifaa vya kutengenezea  kivuko hicho  cha muda vipo  eneo  hilo na kuwa  uwezekano wa kutimiziwa maombi yao ya kupata  huduma  ya  soda na chakula  inawezekana hata kwa  wao wenyewe  kuchangishana kwa ajili ya pesa ya maji .

Alisema  kuwa  Halmashauri ya  wilaya ya  Kilolo na  viongozi wa wilaya  chini ya ofisi  yake  pamoja na mbunge wao Venance  Mwamoto wamekuwa hawalali kutafuta  pesa  kwa  ajili ya kukamilisha ujenzi wa daraja   daraja hilo  na tayari  wizara ya Rais  tawala  wa  mikoa na  serikali  za mitaa (TAMISEMI) imekwisha tenga  bajeti  kiasi  cha  shilingi  milioni 239  kwa  ajili ya ujenzi wa daraja  hilo   na ujenzi huo  utakamilika wakati  wowote .

 

Kuhusu ombi la  wananchi hao  kupatiwa  gari la wagonjwa alisema  ombi  hilo  litafanyiwa kazi   kwani tayari mchakato  wa  kuanza kutafuta gari   hilo  unaendelea  chini ya  ofisi ya  mkurugenzi wa Halmashauri   hiyo.

Mkuu  huyo wa  wilaya  alisema  kuwa  serikali ya  awamu ya  tano ni  serikali ya kazi  na imeendelea  kufanya kazi  zote kwa  faida ya  wananchi na kuwa  changamoto  ni nyingi na imekuwa  ikizitatua changamoto  hizo na  kumpongeza Rais Dkt  John Magufuli kwa  jitihada mbali mbali za  kuwakomboa  watanzania .

Wakati  huo  huo  mkuu  wa  wilaya ameagiza wananchi wa Kiwalamo  kuacha kulalamika njaa kwa  sasa na badala yake  kujikita katika shughuli za kilimo na kupanda mazao ya muda mufupi  badala ya  kuendelea  kulalamika njaa kwa  sasa  wakati mvua  bado zinaendelea  kunyesha katika eneo hilo .
 
Alitaka  wananchi hao  kutumia unyevu unyevu  uliopo  na  mvua  zinazoendelea  kunyesha  kupanda mazao yanayoweza  kufika  badala ya  kuendelea  kulalamika huku vijana  wakishinda  vijiweni huku  wakilalamika  njaa.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE