May 8, 2017

WANAOANDAA MAKUNDI YA UCHAGUZI ,WANAFIKI NA WASALITI WATUPISHE CCM - NAIBU KATIBU MKUU RODRICK MPOGOLO

Naibu  katibu  mkuu  CCM bara  Rodrick Mpogolo  akifungua  warsha  ya  viongozi wa  CCM mkoa  wa Iringa  leo
Wana CCM ambao  ni  viongozi  wakiwa  katika  warsha  hiyo
Mjumbe  wa NEC  kutoka  wilaya ya  Mufindi Marcelina  Mkini kulia  akifuatilia  hotuba ya  naibu  katibu mkuu  CCM Bara  Rodrick Mpogolo
Viongozi  mbali mbali  wakiwa  katika warsha  hiyo

Na  MatukiodaimaBlog
NAIBU  katibu  mkuu  wa  chama  cha mapinduzi  (CCM) bara  Rodrick Mpogolo amesema  chama   hicho  hakitavumilia  mwanachama  yeyote  atakayebainika  kuanza  kuandaa makundi  ya  uchaguzi unaotaraji  kufanyika  ndani ya chama   hicho ama  uchaguzi  mkuu  ujao.

Kwani  alisema   wapo  baadhi ya wana CCM wakiwemo   wabunge  ,madiwani   naadhi ya  watu ambao  wana makundi  yao  ya  kutaka  mtu  furani  kuwa kiongozi ndani ya  CCM jambo  ambalo  halitakiwi na  atakayebainika  kufanya    hivyo atapoteza  sifa ya  kuteuliwa kuwa mgombea  wa nafasi  yeyote  ndani ya  CCM.

Akizungumza  leo  katika  ukumbi wa maendeleo ya  jamii  mjini  Iringa wakati wa   semina ya   viongozi  wa  CCM Mpogolo alisema   kuwa   ili  CCM  kiendelee  kushika  dola  ama  kushinda  kwenye  chaguzi  mbali mbali kwa  kuwa na  viongozi  wasiotokana na makundi  ya  wasaka  pesa ni  vema  wanaoendekeza  makundi  kukaa pembeni  na  kuwapisha  wale  wenye  misingi ya  uongozi bora   kama  ilivyorejesha  amani  kupitia  mwenyekiti  wake  Taifa  Rais  Dkt  John Magufuli .

Kuwa  kupitia  Dkt  Magufuli  chama hicho  kwa  sasa ni  chama  kinachoheshimika  ndani na  nje  ya  nchi  hivyo  ili  imani  hiyo  izidi  na kuwa na viongozi  wenye misingi  ya  uongozi  ni  vizuri  wote  wanaoshindwa  kuvumilia  kufuata  taratibu na misingi ya  uongozi  wa  CCM kuanza kujiengua  wenyewe  kabla ya  kuenguliwa  pindi  watakapobainika  kwenda  kinyume .

Alisema  tayari  kwa  mkoa  wa Iringa  wameshuhudia  jinsi  ambavyo wasaliti  ndani ya  chama  hicho  walivyofukuzwa   na  kuwa  hawatamfumbia  macho  yeyote  anayekichafua  chama   hicho  kwa  kutumia  pesa  zake ama  njia  yeyote  chafu .

Mpogolo  alisema  kuwa   ndani ya  CCM wanahitaji  viongozi  waadilifu  wanaojali  wanachama  na  wananchi  na  sio  viongozi  wanaojali matumbo  yao .

Kuwa kwa  sasa  wapo  madiwani  ,wabunge  ,makatibu na  wenyeviti  ambao  wanapanga  safu  zao  za  uongozi  huku  wakitambua  kuwa  wanabomoa  misingi ya chama   hicho na  kuwa  wenye  wajibu  wa  kupanga  safu  ya uongozi  ni wanachama  wenyewe  kupitia sanduku la  kura  na sio  viongozi  kupitia  pesa  zao .

Hata   hivyo  alisema  kutokana na makundi na  watu  kupanga  safu  zao  ndio  sababu ya kupoteza  jimbo la  Iringa mjini kwenye  uchaguzi  mkuu  uliopita  na  kuwa kwa sasa chama  kitashughulika na  wote  wanaokigawa  chama   hicho  kwa  matakwa yao .

Aidha  alisema  ni  mwiko  kwa  viongozi wa  CCM ama  wanachama  wake  kuwabagua  wagombea ama  kuwapanga kupitia dini  zao ,kabila  ama  rangi  zao na  kuwa  ubaguzi kama   huo hautavumilika ndani ya  CCM hii  ya Dkt  Magufuli .

Pia  alisema  wapo  baadhi ya  viongozi  wa kamati  za siasa  ambao ni  wanafiki na  wafitinishi  ambao  baada ya vikao  hutoka  nje na  kuwagombanisha  wajumbe  jambo ambalo ni baya  zaidi na  kuonya   viongozi  wa  aina  hiyo  kuwapisha ndani ya  chama  hicho  na  kuwa  iwapo  mgombea  yeyote  atathibitika  kuvunja miiko ya  CCM hatapendekezwa  kugombea nafasi  yeyote ndani ya  CCM .

Awali  mkuu wa  mkoa  wa  Iringa Amina  Masenza  akitoa  salamu  zake  katika  mkutano  huo  alisema  kuwa  wapo  baadhi ya  wana CCM ambao  hadi  sasa  wapo  ndani ya chama  ambao ni  wachonganishi na kazi yao  kutengeneza  majungu  dhidi ya  wengine  na  kutaka wembe  uliotumika  kuwanyolea wasaliti  ndani ya  chama  hicho  kuendelea  kuwanyoa wasaliti  waliobaki  ndani ya  CCM.

Alisema  umbea  na majungu yanarudisha  nyuma chama  hicho kwa  baadhi yao  mchana  kuwa ni wana CCM na  usiku wapinzani ambao  wapo  kwa  ajili  ya kuona  CCM inakwama kama  ilivyotokea uchaguzi uliopita  .
 
 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE