May 16, 2017

WAKULIMA WADOGO WADOGO MKOA WA IRINGA EAC IWASAIDIE

Mmiliki wa mtandao   huu wa matukiodaima akiwa shambani kwake
Nyanya  zilizochumwa
Nyanya  zikiwa  zimechumwa
Na MatukiodaimaBlog

WAKULIMA  wadogo wadogo  mkoani Iringa  wameiomba  jumuiya  ya  Afrika  Mashariki (EAC) na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania  kueleza takwimu  sahihi  za faida mpango  wa  EAC  juu ya maendeleo  makubwa ya kilimo barani Afrika chini ya mipango ya CAADP kwa wakulima  wadogo  wadogo .

kizungumza na  waandishi wa habari jana  baada ya kumalizika kwa ukusanyaji wa maoni ya  wananchi  juu ya faida ya   EAC  kwa  wafanyabiashara na wakulima  wadogo wadogo mkoani Iringa   mratibu  wa mradi wa  Iringa Vicil Society (ICISO ) kwa  kushirikiana na The  Foundation For Civili  Society  (FCS)   ,Fadhil Sengele  alisema  kuwa ujumbe  mkuu   wa wakulima  kwa wabunge  wa EAC  ni Pamoja na kukubaliana  na kanuni za (CAAP) na  kuelimishana juu ya  taratibu na maadili ya  mchakato  huo uweze  kunufaisha  wakulima wadogo wadogo .

Pia  wito kwa  ajili ya  kuimarisha  uwekezaji kwa wakulima  wadogo wadogo ,kupunguza  kiwango  cha umasikini kimkoa ,kikanda na kitaifa ifikapo mwaka 2025 kwa njia ya  ukuaji   na mabadiliko makubwa ya kilimo .
Aidha Kuhakikisha  wakulima wadogo wadogo wanashiriki kikamilifu  katika kupanga mipango ya kuongeza kilimo biashara na  jumuiya ya Afrika Mashariki , kuhakikisha  wakulima  wadogo wadogo  wanawezeshwa  juu ya namna ya  kuboresha maisha ya familia  zao na namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi  ili  waweze  kulima kilimo chenye tija  na kuhakikisha uwajibikaji  wa Pamoja kwa hatua zilizofikiwa ili kupata matokeo  tarajiwa katika sekta ya  kilimo na biashara .

Mratibu huyo alisema wakulima wadogo wadogo  mkoani Iringa  wameshindwa kushiriki na kufaidika na EAC kwa sababu ya  kukosa taarifa  na uwezeshaji wa  jinsi ya kufanya  biashara na kupata  masoko  ya EAC  hivyo wanaomba  jumuiya hiyo  na serikali ya  Tanzania  kuweka  mkakati  wa Pamoja wa  kuwasaidia wakulima  wadogo kunufaika na soko hilo kwa  kufungua madirisha ya  kibiashara  kwa  kuwaeleza  fursa za  biashara  zinazopatikana  kwa urahisi kwa wao kuvuka mpaka  wa nchi .

“ kuna  haja ya kutoa maelekezo  ya kina ya  jumuiya ya Afrika Mashariki  kwani ni  vitu  vinavyoweza  kusaidia  wakulima  wadogo wadogo  ushiriki katika  biashara  ndani ya masoko  yaliyopo  EAC”
Alisema  kuwa  wakulima  hao  wanaiomba  serikali  ya Tanzania kutambua  kuwa  wakulima  wadogo wadogo  wanatakiwa kuandaliwa utaratibu  wa  uwezeshwaji na  kujengewa  mitandao  ya uhakika na mashirika tofauti  ili  kuwawezesha  kujitegemea kiutendaji  kwa maendeleo ya Taifa kwa  wao kushiriki katika  masoko ya EAC .

Kuwa mchakato wa  ushirikiano kutoka  serikalini na sekretarieti ya  EAC  zina wajibu  wa  kukuza uelewa   kwa  kuhakikisha  ufanisi  wa  kibiashara wa mazao ya kilimo na katika kufanya maamuzi ya moja kwa moja  kwenye mambo ya msingi yanayohusu mtangamano  huo .

Hivyo wito  wa  wakulima  hao kwa  wajumbe wa EAC  ni  kushawishi  uwezeshaji wa haraka kwa  wakulima  na  wadfanyabiashara   wadogo  wadogo nchini  kuelimishwa  juu ya uzalishaji wa mazao yenye ushindani wa kibiashara  ili  kunuifaika na soko la EAC  na kuwawezesha  kutumia itifaki za EAC  kama umoja  wa  forodha  na itifaki ya soko la Pamoja .

Aidha alisema  serikali ya  Tanzania  na sekretarieti ya EAC   zinapaswa  kutambua kuwa  wakulima  wadogo wadogo  wana ukaribu wa mitandao  na mashirka mbali mbali hivyo  kinachotakiwa ni  uwezeshaji kwa  wakulima  ili  waweze kukuza umiliki wa  mitaji yao.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE