May 19, 2017

WAFUNGWA ZAIDI WATOROKA JELA LA KINSHASA

         Magari yaliyokuwa yameegeshwa karibu na gereza la Kinshasa yalichomwa moto Jumatano                                              Magari yaliyokuwa yameegeshwa karibu na gereza la Kinshasa yalichomwa moto Jumatano                

Wafungwa wengine wametoroka kutoka gerezaji siku mbili baada ya zaidi ya wafungwa 3,000 kutoroka kwenye gereza kuu nchini humo.

Wafungwa 60 wanadaiwa kutoroka kutoka jela ya Kasangulu, kilomita 40 kutoka mji mkuu Kinshasa.
Gereza hilo linapatikana katika eneo ambalo ni ngome ya madhehebu ya Bundu Dia Kongo.


Katika kisa cha awali, ambapo wafungwa wengi walitoroka gereza kuu mjini Kinshasa, kiongozi wa madhehebu hayo aliyekuwa amezuiliwa anadaiwa kuwa miongoni mwa waliofanikiwa kutoroka baada ya watu wenye silaha kuvamia jela hiyo.


Kwa sasa, maafisa wa serikali watafakari uwezekano wa kutuma jeshi kulinda magereza.(Chanzo BBC)

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE