May 1, 2017

WAFANYAKAZI IRINGA WAOMBA KIMA CHA CHINI KIWE 750,000

wafanyakazi  Iringa  wakiwa katika maandamano yao
wafanyakazi  wakiandamana  kwenda viwanja vya maadhimisho
wafanyakazi Iringa wakiwa na bango linaloomba nyongeza za  mishahara
Mbunge wa viti maalum mkoa  wa Iringa Ritta Kabati  akitoa  salama mbele ya wafanyakazi
mkuu  wa wilaya ya  Mufindi  Jamhuri Wiliam akisalimia
Mkuu  wa wilaya ya  kilolo Asia Abdalah
Mratibu  wa maadhimisho hayo Bw Magessa  akisoma risala ya  wafanyakazi
Rc Iringa Amina Masenza  akitoa zawadi
r="0" height="426" src="https://2.bp.blogspot.com/-VNZkp2-G8vE/WQdGTytv23I/AAAAAAACcxM/EEJ6bdWfrT0l2vdmax0Z_JIoz6qTOEwTwCLcB/s640/DSC_0175.JPG" width="640" />
WAFANYAKAZI mkoa wa Iringa wapinga zoezi la utumbuaji majipu kwa upendeleo kuwa zoezi hilo linaleta ubaguzi na kutaka zoezi hilo kuendelea bila kutazama sura ya mtu.

Pamoja na kutaka wanaopaswa kutumbuliwa watumbuliwe pasipo huruma pia wametaka zoezi la vyeti feki liendeshwe kwa haki.

Wakisoma risala yao leo  wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya kichangani mjini Iringa, mbele ya mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza walisema kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano ya hapa kazi tu italeta tija kama hakutakuwa na ubaguzi katika maamuzi mbali mbali.

Mratibu wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi (TUCTA)  mkoa wa Iringa Deus Magessa alisema kuwa wafanyakazi mkoa wa Iringa wanaunga mkono uamuzi wa kuwepo kwa kauli mbio ya Hapa kazi Tu na kuitekeleza kwa vitendo ili kuleta tija na maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Aidha alisema wanapinga vikali mazoea ya baadhi ya viongozi wa juu ya uvunjwaji wa kanuni taratibu na sheria za kazi katika kuwaadhibu watumishi maarufu kama utumbuaji majipu.

Kuwa zoezi hilo linasababisha maeneo ya kazi wafanyakazi kutokuwa na amani utulivu na uhakika wa ajira zao.

Hivyo alisema wanaishauri serikali na waajiri wengine wasiingie kwenye migogoro na vyama vya wafanyakazi kwa kutofuata Sheria, kanuni na taratibu za upandishwaji na ushushwaji wa madaraja ya wafanyakazi.

Walisema wao kama wafanyakazi mkoa wa Iringa wanapinga na kulaani vikali sheria ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu kuhusu kuwakata asilimia 15 wale waliosaini mikataba na bodi kukatwa asilimia 8 kwa sababu wao hawajawahi kusaini makubaliano ya kukatwa asilimia 15.

Alisema kupitia sherehe hizi wanaitaka serikali kuhakikisha bodi za kutathimini kima cha chini cha mshahara kwa sekta binafsi na umma kinawajibika kufanya hivyo kwani kima cha chini cha mshahara bado hakikidhi matakwa na mfanyakazi.

Alisema ni vema sasa bodi husika kuishauri serikali ili kuongeza kima cha chini japo kufikia shilingi 750,000 bila kufanya hivyo wataitisha mgomo usio na kikomo hadi kilio chao kitakapopatiwa jibu.

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza aliwataka wafanyakazi hao kufanya kazi kwa kutimiza wajibu wao huku akiwataka waajiri kutoa motisha kwa wafanyakazi wanaofanya vizuri.

Kuwa vyama vya wafanyakazi vinawajibu mkubwa wa ustawi wa wafanyakazi wao na waajiri unakuwepo, hivyo vyama vinatakiwa kuhakikisha watumishi wanapata elimu zinazohusiana na masuala mbali mbali.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE