May 26, 2017

WACHIMBAJI WADOGO MADINI NYAKAVANGALA WAANZA KUPEWA LESENIImage result for madini wachimbaji  wadogoWAKATI  ukiwa ni mwezi mmoja sasa  toka  wachimbaji  wadogowadogo  zaidi ya 500  kuvamia  eneo la  kijiji  cha Nyakavangala tarafa ya  Ismani  wilaya ya  Iringa  mkoani Iringa  kufanya  shughuli za uchimbaji wa madini ya  dhahabu  ofisi ya kamishina wa madini kanda ya  nyanda za  juu kusini imetoa leseni ya uchimbaji wa madini kwa mchimbaji mmoja ili  kuendelea  kufanya  shughuli za  uchimbaji wa  madini hayo katika eneo hilo.

Akizungumza baada ya  kukabidhiwa  leseni ya  uchimbaji wa madini  eneo hilo jana mchimbaji Thomas Masuka  alisema  kuwa  ameanza kazi hiyo ya  uchimbaji wa madini  katika maeneo mbali mbali  toka mwaka 1993  na ana uzoefu mkubwa wa uchimbaji wa madini na namna ya  kuwasaidia  wananchiwanaozunguka eneo lake la  uwekezaji  kutatua  changamotozinazowazunguka .

Masuka  alisema  kuwa amepata kuifanya kazi  hiyo ya  uchimbaji madini katika wilaya ya Bai mkoa wa Dodoma Wilaya ya Handeni  mkoa wa Tanga ,wilaya ya Nyanumbu mkoa wa Mtwara na maeneo  mengine  mengi ya nchi  ya Tanzania .
Image result for RAis  wachimbaji madini wadogo Bina
Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA),Alisema  kuwa pamoja na uwekezaji wake  wauchimbaji wa madini katika  eneo  hilo umeanza kuwanufaisha  vijana na  wananchi  zaidi ya 6000  ambao  wanajishughulisha na biashara  mbali mbali na baadhi yao  wanafanya kazi  kwenye  mgodi  huo bado ataendelea  kufanya kazi  hiyo kwa  mujibu wa sheria za  nchi na sheria za madini kwa  kulipa kodi ya serikali  asilimia 0.3 ya  halmashauri ,asilimia 4 ya Mrahabara wa  serikali  kuu ,kodi ya  leseni na makusanyo yote yanayotokana eneo la mgodi asilimia 30  kwa  ajili ya kijiji hicho .Masuka  alisema  kuwa kwa wakati  wote ambao atakuwa akishughulika na  shughuli ya  uchimbaji wa madini ya  dhahabu  eneo  hilo la Nyakavangala atahakikisha  anafanya  kazi  zakekwa  ushirikiano  mkubwa  nawananchi  wa  eneo  hilo .Hadi   hivi  sasa idadi ya  wachimbaji wadogo  wadogo  wasio na vibali  wameendelea kuongezeka  kila kukicha katika  eneo  hilo la Nyakavangala huku  mbali ya mchimbaji Masuka  kupewa  kibali jumla ya  wachimbaji  wadogo  sabawalituma maombi kanda ya kuomba  leseni ya uchimbaji wa madini ila  ni mmoja pekee ndie  aliyefanikiwa  kupewa  kibalikutokana na kukidhi  sifa  za uchimbaji wa madini .Mkuu wa  mkoa  wa  Iringa Amina Masenza alisema  kuwa tayari  amekwisha  iagiza kamati yake ya  ulinzi wa usalama ikiongozwa na kamanda wa  polisi mkoa wa Iringa Julius Mjengi  kufika eneo hilo ambalo wachimbaji  wadogo  wadogowamevamia na kuifanya kazi hiyo  kiholela na baada ya hapo  atakutana na kamishina wa madini kanda ili  kuona namna gani ya kufanya shughuli hiyo kwa  kuzingatia sheria  ya  uchimbaji mdogo  mdogo wa madini.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE