May 18, 2017

TUIANZE SIKU NA MUNGU...


Isaya 54:17:

Kila silaha itakayofanyika juu  yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako ktk hukumu utahukumiwa kuwa mkosa,huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana na Haki yangu inayotoka kwangu Mimi Asema Bwana.


Mwenyezi Mungu utupaye uzima na utulindae na yote tunasema ahsante kwa ulinzi wako na ahsante kwa kuiona siku mpya.

Kwani wewe Mungu u mwamba wa makazi yangu ,hivyo Mungu tunaomba wainue wote wakutegemeao wewe katika maisha yao.

Tunakuja kwako kuwaombea wasafiri wote wanasafiri siku ya Leo Mungu waongoze na waponye wagonjwa wote Mungu.

Twasogea mbele ya kiti chako Mungu tukiomba iguse mioyo yetu na maisha yetu tukutumaini wewe na tuongoze tunapokosea zaidi ya tote Mungu tunaomba tembea nasi na shinda nasi popote pale .

Shetani hana mamlaka na miili yetu wala mipango yetu twaomba tusaidie kutuepusha na Matukio yote  ya kinyama na tunakemea kwa nguvu zote mauwaji yanayoendelea huko Kibiti Mungu pekee yetu hatuwezi kushinda haya ila  kwa nguvu zako Mungu tunasema yatosha kuendelea kusikia unyama huu.

Mungu baba tunaomba ulinzi na Baraka kwa serikali yetu na viongozi wake wote watuongoze kama wewe Mungu utakavyo na waweze kukutanguliza wewe Mungu

AMEN

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE