May 17, 2017

MSANII DOGO MFAUME ALIYEIMBA KAZI YANGU YA DUKANI AFARIKI DUNIA

Msanii Dogo Mfaume  Enzi za  uhai  wake 
                                                            Na  MatukiodaimaBlog
Kama sikio lako huzitegea sana nyimbo za bongofleva basi na ‘kazi ya dukani’ inaweza kuwa moja ya zile unazozijua…. na ni ngoma ambayo ilifanywa na Msanii aitwae Dogo Mfaume ambaye leo tumepokea taarifa za kifo chake Muhimbili Hospital.

Mmiliki wa Sobber House alikokua akisaidiwa ili kuachana na utumiaji wa dawa za kulevya amesema ‘alikua afanyiwe upasuaji Ijumaa kutokana na uvimbe kwenye ubongo na alikua tayari ameshapangwa kwenye ratiba’

‘Afya yake ilikua nzuri kabisa na alikua ana mwaka mmoja toka ameacha utumiaji wa dawa za kulevya ‘unga’ na tulikua tumejiandaa kesho twende tukamtolee damu’

Akiongea huku analia Mmiliki huyo wa Sobber House ameendelea kueleza ‘Afya yake ilikua nzuri kabisa na aliniambia dada mimi sitaki kuondoka kwako nataka unisimamie kila kitu na sitaki kurudi mtaani, mtaani hali mbaya na nikikaa kule nitarudi kutumia unga”

“Aliniambia naomba nisimamie tu mimi nakaa hapahapa…… masikini ya Mungu huu uvimbe eeeh Mungu jamani… amefariki na wameshamzungushia na kile kitambaa cha kijani‘

R.I.P Dogo Mfaume

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE