May 19, 2017

SOMA HAPA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI WALIOPOTEZA MAISHA KTK MGODINI KWA KUKOSA HEWA IRIRINGA

Wananchi wa Msuluti kata ya Magulilwa   wilaya ya  Iringa  wakiwa wamebeba mmoja kati ya  miili ya  wachimbaji  wadogo  wawili  waliokufa mgodini kwa  kukosa hewa  leo
Miili  ya  wachimbaji  wadogo  wawili katika mgodi ya Mamweli Msigwa  ukiingizwa  kwenye  gari la polisi
Kamanda  wa  polisi mkoa wa Iringa Julius Mjengi katikati mwenye kofia nyeusi  akionyeshwa shimo   la mdogi  wa dhahabu ambalo  limesababisha  vifo  vya watu  wawili
Wananchi  wakiwa  eneo la tukio
Askari   polisi na wananchi  wakitazama mgodi  huo uliouwa
Milili  ya  wachimbaji  wadogo  wawili  walipoteza maisha  mgodini  leo
Kamanda  wa  polisi  mkoa  wa Iringa  Julius Mjengi kushoto akitazama shimo la mgodi  katika  kijiji  cha Msuluti  kata ya Magulilwa wilaya ya Iringa ambalo wachimbaji  wawili  wadogo wawili  walipoteza maisha kwa  kukosa  hewa wakati  wakichimba madini leo asubuhi
Mmiliki wa mgodi huo Samweli Msigwa kushoto akihojiwa na polisi ,katikati ni kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Julius Mjengi
 Kamanda  wa  polisi  mkoa  wa Iringa  Julius Mjengi kushoto akitazama shimo la mgodi  katika  kijiji  cha Msuluti  kata ya Magulilwa wilaya ya Iringa ambalo wachimbaji  wawili  wadogo wawili  walipoteza maisha kwa  kukosa  hewa wakati  wakichimba madini jana asubuhi
....................................................................................................................................................................
 Na MatukiodaimaBlog
WACHIMBAJI wawili  wadogo wa madini ya dhahabu katika kijiji cha Masuluti kata ya Magulilwa tarafa ya Mlowa wilaya ya Iringa mkoani Iringa wamefariki dunia baada ya kukosa hewa ndani ya mgodi.

Akizungumzia tukio hilo afisa mtendaji wa kijiji cha Masuluti Venjaslaus Kiunosile alisema kuwa tukio hilo  limetokea Leo Majira ya saa  5 asubuhi.

Alisema kuwa taarifa ya tukio hilo alipewa na mchimbaji mwenzao aliyewatembelea marehemu hao kwa ajili ya kuwasalimia.

Mtendaji huyo alisema kutokana na taarifa hiyo walilazimika kutoa taarifa polisi .

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Julius Mjengi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa miili ya marehemu hao imetolewa katika mgodi huo.

Aliwataja waliofariki dunia kwa kukosa hewa kuwa ni Haus Kaijage (32) mkazi wa Bukoba na James Mlawa(22) mkazi wa Magulilwa.

Alisema chanzo cha watu hao kupoteza maisha ni kukosa hewa baada ya kuingiza jenereta la kuvuta maji mgodini kwa lengo la kuvuta maji na baada ya kuliwasha walikosa hewa.

Hata hivyo alisema alisema wachimbaji hao walichukua mashine hiyo na kuingiza ndani na mgodi baada ya awali kuharibika na kuwa jeshi la polisi linamshikilia kwa mahojiano mmiliki wa mgodi huo Samweli Msigwa.

Kamanda Mjengi alitoa wito kwa wachimbaji wadogo katika mkoa wa Iringa kuzingatia usalama katika uchimbaji wa madini.

Kwa upande wake Mganga mfawidhi wa kituo cha afya Mgama Dkt Baraka Mwifune alisema uchunguzi alioufanya unaonyesha  watu hao walipoteza maisha kwa kukosa hewa.

Mmiliki wa mgodi huo Samweli Msigwa alisema kuwa akiwa njiani kuelekea eneo la mgodi kwa ajili ya kusaidia kutengeneza machine ya kuingiza hewa katika mgodi huo ndipo alipopata taarifa ya wachimbaji hao wawili kati ya Sita kupoteza maisha kwa kukosa hewa.

Alisema mgodi huo ulikuwa na wachimba   Sita kabla ya wanne kwenda mgodi mpya wa Ismani na hivyo walibaki hao wawili na kuwa anamiliki mgodi huo kihalali na ana kibali kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.
Mwisho

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE