May 3, 2017

SIMBA BADO WALIA NA POINTI 3 ZA KAGERA


Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva jumatano ya Mei, 3 amezungumza na waandishi wa habari kuhusu mambo mbalimbali ambayo yanendelea katika klabu hiyo. Baadhi ya mambo hayo ni kuhusu Kagera Sugar kurudishiwa alama tatu, Fainali ya Kombe la FA, kufungiwa kwa Haji Manara na maamuzi ambayo yanafanywa na Kamati ya sheria na hadhi za wachezaji.
Alichosema Aveva kuhusu Kagera Sugar kurudishiwa alama tatu, “Simba ilitakiwa ipewe alama tatu, Kagera waliomba review lakini ikaenda kwenye kamati nyingine na kamati ikaona kulikuwa na makosa kwenye kamati ya masaa 72 na ikatoa maelezo yake lakini ukiangalia mantaki ya maamuzi yale ni Simba haistahili kupata zile alama tatu,
“Sababu iliyotajwa ni kuwa ilipeleka nje ya muda maombi, malalamiko ilibidi ipeleke na ada ya 300,000 na kikao cha masaa kamati ya 72 kilijumuisha mjumbe ambaye si halali, kwa sababu hizo kamati ikaona si jambo jema Kagera kuporwa zile pointi,
“Sisi kama Simba tunaona hii sio sawa na sio sawa hata kidogo Simba hatuwezi kukaa kimya, niwaombe wanachama na mashabiki wakae kimya, tunasubiri barua ya bodi, tunachotaka kusema zile pointi tatu ni mali ya Simba, kuna mkanganyiko kati ya bodi na kamati ya sheria na hadhi kwani waliyozungumza ilitakiwa yawe maoni kwenda kwenye bodi,
“Tumefanya tathmini kwa kina, tumeulizia njia ya kupita tumeambiwa tunaweza kwenda FIFA, uamuzi wa Simba tutalipeleka jambo hili FIFA, huko sasa ndiyo tutapata haki yetu, tumeambiwa kuna gharama inaweza fika hata Dola 15,000 lakini tutalishughulikia, tunasubiri barua ya bodi,
“Taratibu za FIFA zipo wazi wakati jambo letu linazungumzwa ki taratibu bodi inatakiwa kusimamisha matokeo ya mechi hiyo hadi majibu yatakapokuja kutoka CAF, kwahiyo Wanasimba popote walipo tuwe watulivu tuone uongozi unafanya nini kwenda FIFA.”
Kuhusu fainali ya Kombe la FA kati ya Simba na Mbao FC,
”Tulipata kigugumizi kuwa mchezo kama ule unafanyiwa droo ya kutafuta uwanja wa kuchezewa mchezo wa fainali, sisi kama Simba tunatoa rai moja tu kwa waendeshaji na wadhamini unaposema FA unatafuta bingwa wa kushiriki mashindano ya kimataifa, tuwe tunapewa ratiba kabisa ya viwanja, ni mashindano makubwa
haya,
“Sisi Simba tunaona kuna kitu kilikuwa wanataka kutengeneza, lilikuwa ni swala la kutufahamisha mapema lakini kufanya droo lingetuchanganya, sisi hatuna shida na Dodoma watatukuta tumetangulia, tunawaheshimu Mbao lakini hatuwaogopi, tunategemea pambano litakuwa zuri, hata wangesema Kirumba au Nyamagana tungecheza.”
Kuhusu kufungiwa kwa Haji Manara, ”Amefungiwa barua haijasema amefungiwa nini, imesema tu amefungiwa mwaka mmoja na faini ya milioni tisa, bwana Haji alifanya press ya Simba, inaonekana alizungumza maneno ya kukera watu na shirikisho hivyo wakamchukulia hatua,
“Aliomba likizo ya muda mfupi kutoka kwa mwajiri na mimi kama mwajiri nilimruhusu ndiyo ile barua ikaja ikimtaka Haji, na mimi nikawataarifu TFF hayupo hivyo wasogeze mbele hadi arudi, na wakati huo Haji yupo nje ya Dar lakini kilifanyika kikao na wakatoa maamuzi hayo.
“Kuna uharaka sana wa kuchukulia ishu ya Haji kutoa maamuzi haraka hivyo, tunauzoefu watu wa Simba tuna kesi nyingi tumepeleka TFF hadi leo hazijafanyiwa kazi, tumemwomba Haji apelike review TFF na amefanya hivyo na malipo yote yamefanyika hivyo tunataraji muda wowote ataitwa na yeye akajitetee.”
Kuhusu maamuzi ambayo yanafanywa na Kamati ya sheria na hadhi za wachezaji ,”Tumekuwa hatupati haki katika mambo mengi ya kimsingi ambayo tunapeleka TFF, mifano hai tunayo, tuna kesi ya Singano hadi leo haina ufumbuzi na kesi ya usajili wa mchezaji Mbaraka Yusuph, sisi tulimtoa kwenda Kagera, msimu wa 2016/17 ilikuwa arudi kuchezea Simba, na TFF iliidhinisha Mbaraka kuchezea Simba,

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE