May 7, 2017

SAMIA KUONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA WANAFUNZI WALIOFARIKI DUNIA MKOANI ARUSHA

 
Makamu wa Rais, Samia Suluhu kesho saa mbili asubuhi ataongoza wakazi wa Arusha katika Uwanja wa Sheikh Abeid Karume kuaga miili ya wanafunzi waliofariki katika ajali ya gari Arusha ambapo serikali imegharamia sanda  na majeneza kwa wanafunzi wa shule Lucky Vincent waliopoteza maisha jana kwenye ajali.

Akitoa taarifa hiyo leo Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro,  amesema taarifa za awali zinaonyesha tayari serikali imekwishalipia gharama za majeneza na sanda za kuhifadhia miili ya marehemu ambao kesho wanatarajiwa kufanyiwa ibada katika Uwanja wa heikh Amri Abeid.
Mazingira ya shule hiyo.
Aidha Lazaro amesema viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri na wabunge bado wanaendelea kukusanyika katika eneo la shule ya Lucky Vincent  kwa ajili ya kikao.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE