May 26, 2017

TCRA YAVIKUMBUSHA VYOMBO VYA UTANGAZAJI KUZINGATIA SHERIA NA KANUNI YA UTANGAZAJI

JAMHURI YA YA MUUNGANO YA TANZANIA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA TAARIFA KWA UMMA KUFUATA SHERIA NA KANUNI ZA UTANGAZAJI

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inavikumbusha vyombo vya habari vya utangazaji nchini kufuata na kuzingatia Sheria na Kanuni za Utangazaji zinazoiongoza sekta kwa manufaa na ustawi wa nchi yetu.

Kwa mujibu wa Sheria na. 12 ya mwaka 2003 TCRA imepewa dhamana ya kusimamia sekta ya Mawasiliano nchini ikiwa ni pamoja na masuala yote ya Utangazaji. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania haitakivumilia chombo chochote cha utangazaji kitakachokiuka miongozo ambayo imo katika Sheria Na. 10 ya 2010 ambayo ni Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta na Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari Tanzania, 2016 .

 Mamlaka pia inavitaka vyombo vya utangazaji kuzingatia kanuni za utangazaji za 2005 zilizowekwa kusimamia sekta. Hii ikiwa ni pamoja na Kanuni zinazosimamia uwasilishaji wa vipindi vya Radio na Televisheni vya kila robo mwaka kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na matangazo ya moja kwa moja (Live programs) kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni 22(1),(2) na (10).

Hatua stahiki zitachukulia iwapo ukiukwaji utatokea. Aidha Mamlaka inawataka wale wote ambao wanaona wanaathiriwa kwa namna moja au nyingine na maudhui yanayorushwa na kituo chochote cha utangazaji kupeleka malalamiko yao kwa njia ya maandishi kwa kituo husika na kuleta nakala ya malalamiko hayo TCRA kwa ajili ya taarifa na ufuatiliaji zaidi.

 Nakala ya Malalamiko hayo itumwe kwa:

Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, S.L.P 474, 20 Barabara ya Sam Nujoma,

 14414, Dar es Salaam.

TANZANIA. IMETOLEWA NA: MKURUGENZI MKUU MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA 26 MEI, 2017 ISO 9001:2008 CERTIFIED

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE