
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akiongozana na Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dkt. Tausi
Kido walipokuwa wakielekea katika uzinduzi wa mafunzo yahusuyo Radio ya
Jamii kwa Maendeleo Vijijini yaliyofanyika Mjini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dkt. Tausi Kido akitoa hotuba ya
utangulizi wakati wa uzinduzi wa mafunzo yahusuyo Radio ya Jamii kwa
Maendeleo Vijijini yaliyofanyika Mjini Dodoma.

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akizungumza na washiriki wa
mafunzo (hawapo pichani) yahusuyo Radio ya Jamii kwa Maendeleo Vijijini
yaliyofanyika Mjini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo
yahusuyo Radio ya Jamii kwa Maendeleo Vijijini wakimsikiliza Naibu
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (
hayupo Pichani) yaliyofanyika Mjini Dodoma.

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akiwa katika picha ya pamoja na
washirki wa mafunzo yahusuyo Radio ya Jamii kwa Maendeleo Vijijini
yaliyofanyika Mjini Dodoma.
Picha na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma.
Na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma
24/05/2017
Redio za jamii nchini zimeshauriwa
kutotumiwa na wanasiasa katika uendeshaji wa kazi zao bali zizingatie
dhumuni kuu la kuelimisha wanajamii katika kuleta maendeleo ya Jamii.
Hayo yamesemwa na leo Mjini Dodoma
na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe, Anastazia
Wambura alipokuwa akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo yahusuyo Radio
ya Jamii kwa Maendeleo Vijijini kwa waandishi wa habari, wawakilishi
kutoka Halmashauri za Wilaya nchini yaliyofanyika Mjini Dodoma.
Mhe. Anstazia Wambura amesema kuwa
Redio za Jamii zinatakiwa kusimamia malengo yao makuu ya kuwa karibu na
jamii husika na kuzifanya jamii hizo kunufaika na Redio hizo na sio
kufarakanisha jamii.
“ Nisistizie kwa washiriki
kuzingatia malengo ya mafunzo haya mnayopewa ili yasaidie katika
kuielimisha jamii katika masuala mbalimb ali na kuachana na masuala ya
siasa” Alisistiza Mhe. Anastazia.
Mhe. Anastazia Wambura amesisitiza
kuwa wataalamu wa habari wanatakiwa kutumiwa vizuri katika Halmasahuri
nchini ili kuzisaidia Redio za Jamii ziweze kufanya kazi yao kwa ufanisi
zaidi.
Waandishi wa habari kutoka katika
Redio za jamii nchini pamoja na wawakilishi kutoka Hamlashauri za Wilaya
nchini wapo katoika mafunzo ya siku mbili yahusuyo Radio ya Jamii kwa
Maendeleo Vijijini yanayofanyika Mjini Dodoma.
0 comments:
Post a Comment
AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE