Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Julius Mjengi |
............................................................................................................................................................
Na Matukiodaima Blog
JESHI la polisi mkoa wa Iringa limemkamata mtuhumiwa wa biashara za dawa ya kulevya pamoja na mteja wake aliyekuwa katika harakati za kununua dawa hizo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Julius Mjengi aliueleza mtandao huu wa matukio daima ofisini kwake leo kuwa mfanyabiashara huyo Ramadhan Abduli (38) mkazi wa Ilula katika wilaya ya Kilolo alikamatwa jana majira ya saa 12.30 jioni akiwa anaandaa kete 30 za dawa za kulevya aina ya Heron na bangi kete 195.
Alisema kuwa mtuhumiwa huyo alikutwandani ya Pagale akifunga kete hizo huku mteja wake Hamza Adamu (36) akinunua dawa hizo.
Kamanda Mjengi alisema pamoja na mfanyabiashara huyo kukamatwa na dawa hizo pia alikamatwa na pesa kiasi cha shilingi 282,300 ambazo ni fedha zilizotokana na mauzo ya dawa hizo.
Alisema kuwa watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa baada ya upelelezi wa kesi hiyo kukamilika .
Hata hivyo alisema kuwa jeshi la polisi mkoa wa Iringa limejipanga kuendesha msako wa kuwasaka wale wote wanaojihusisha na biashara ya dawa za kuevya na watumuaji wa dawa hizo na kuwachukulia hatua kali .
Kamanda huyo alitoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa kuwafichua wale wote wanaojihusisha na matukio mbali mbali yakiwemo ya uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya .
0 comments:
Post a Comment
AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE