May 27, 2017

RITTA KABATI CUP KUFUNGULIWA NA WAZIRI DKT MWAKYEMBE LEO IRINGAImage result for mbunge  kabati  michezo
Mbunge Ritta  Kabati akipiga mpiga
.......................................................................................................................................................................
WAZIRI wa habari,utamaduni,sana na michezo Dkt  Harrison Mwakyembe leo  kuzindua Mashindano ya Ritta Kabati challenge cup .


Mratibu wa mashindano haya Fredy Mgunda alisema  kuwa maandalizi yote ya uzinduzi wa mashindano hayo yamekamilika.

Alisema kuwa uzinduzi huo utafanyika katika uwanja wa Chuo cha Kreluu mjini Iringa Hata hivyo alisema kuwa lengo la mashindano hayo ni kuibua vipaji vya soka  na fursa kwa timu ya Lipuli Fc ambayo imepanda ligi kuu kupata wachezaji kupitia mashindano hayo.

Kwani alisema timu zote zinazoshiriki zimeonyesha kuwa na wachezaji wenye  uwezo mkubwa wa kutambiana katika mashindano hayo.

Katika mashindano hayo bingwa ataondoka na piki piki,mshindi wa pili mashine ya kufyatua tofali na mshindi wa tatu atapewa kombe.Kwa upande wake mratibu wa mwandaaji wa mashindano hayo mbunge Kabati alisema mashindano hayo maalum kwa vijana wote na hayana itikadi ya CCM pamoja na kuwa yeye ni mbunge wa   CCM.Alisema kusudi lake kuona michezo ndani ya mkoa inapewa kipaunbele na vijana hawashindi vijiweni bila kufanya kazi.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE