May 24, 2017

PANDA SHUKA YA PROFESA MUHONGO

 
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amepitia misukosuko katika nafasi za uwaziri tangu alipoteuliwa na Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete.
 Leo Rais John Magufuli amemtaka Profesa Muhongo ajitathmini kuhusu nafasi yake ya Uwaziri baada ya kupokea ripoti ya mchanga wa madini Ikulu.
Mei 2012, Rais Kikwete alimteua Muhongo kuwa mbunge pamoja na wabunge wengine watatu, akiwamo Janet Mbene na James Mbatia.
Baada ya kuteuliwa na kuwa mbunge, Muhongo aliteuliwa na kuwa Waziri wa Nishati na Madini  na Rais Kikwete.
Hata hivyo Januari 24 mwaka 2015, alimuandikia Rais barua ya kujiuzulu kutokana na sakata la uchotwaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.
Mwaka mmoja baadaye, baada ya Rais John Magufuli kuingia madarakani, alimteua tena Profesa Muhongo kuwa Waziri wa Nishati na Madini.
Muhongo alishinda kiti cha ubunge wa Jimbo la Musoma Vijijini kwa tiketi ya CCM, katika uchaguzi wa 2015.
Lakini leo tena, ikiwa ni miaka zaidi ya miwili tangu ajiuzulu kutokana na kashfa ya Escrow, ametakiwa kujiuzulu kutokana na  sakata la mchanga wa madini.
#Mwananchi

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE